TAASISI ZA SEKTA YA UCHUKUZI ZA SERIKALI NA WADAU BINAFSI ZATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WEREDI NA KUSHIRIKIANA ILI KUKUZA UCHUMI WA TAIFA.

12 Apr, 2023
TAASISI ZA SEKTA YA UCHUKUZI ZA SERIKALI NA  WADAU BINAFSI ZATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WEREDI NA KUSHIRIKIANA ILI KUKUZA UCHUMI WA TAIFA.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Prof.Makame Mbarawa Leo amezitaka Taasisi na Wakala za Serikali na Binafsi kufanya kazi Kwa weredi na kushirikiana ili kuboresha Sekta ya Uchukuzi katika kukuza UCHUMI wa Taifa kwani Serikali inathamini uchagizaji wa Maendeleo wa Sekta hizo katika kuinua UCHUMI.

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Makame amesema hayo Leo kwenye ukumbi wa JNICC _Dar Es salaam wakati wa majadiliano ya Wizara (Sekta ya Uchukuzi) na wadau wa Sekta Binafsi ulilolenga kutambua fursa,changamoto na mapendekezo ya maboresho kuhusu Maendeleo ya Sekta ya Uchukuzi, yaliyobebwa na kauli mbiu ya "UCHUKUZI KWA UKUAJI ENDELEVU WA UCHUMI".

Wataalamu kutoka Chuo Cha Bahari Dar eS Salaam (DMI) wakiongozwa na Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt.Tumaini Gurumo, wameshiriki mkutano huo kama wadau wa Sekta ya Uchukuzi upande wa Baharini na Majini ili kujipanga kimkakati kuhakikisha lengo la Serikali linafikiwa Kwa kutoa Elimu na Mafunzo Bora hatimae kupata wataalamu wazuri kwenye Sekta hiyo.

 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Prof.Makame Mbarawa akizungumza na wadau wa sekta ya uchukuzi wa Serikalini na Binafsi.

 

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo (katikati), kushoto ni Mku wa Chuo cha usafirishaji NIT Prof.Zacharia Mganilwa wakifuatilia kwa makini mjadiliano ya mkutano.

Wataalamu wa DMI wakifuatilia kwa makaini majadiliano  yanayoendeshwa kwenye ukumbi kuhusianan na namna ya Kuboresha Sekta ya Uchukuzi kwa kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Taifa letu.

Mkutano ukiendelea.

meza kuu wakiongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Prof Makame Mbrawa wakifuatilia uwasilishwaji wa hoja kutoka sekta za umma na binafsi kwa lengo la kuiboresha Sekta ya Uchukuzi.