Huduma za TEHAMA

Huduma za TEHAMA zinazotolewa na Kitengo cha TEHAMA ni kama ifuatavyo

1) Huduma ya Intaneti

Kitengo kinawajibu wa kuhakikisha Ofisi na Maabara za Kompyuta zinapata huduma ya Intaneti kwa watumishi pamoja na Wanafunzi, kuna idadi ya kompyuta zaidi 150 ambazo tunazihudumia kupata Intaneti.

2) Matengenezo ya Kompyuta na programu zake

Kitengo kinatoa huduma ya Matengenezo ya Vifaa vya Kompyuta pindi panapotokea tatizo na kutoa ushauri wa Matumizi sahihi ya Vifaa pamoja na Programu za Kompyuta, kwa kuzingatia waraka wa Utumishi Na.5 wa mwaka 2009 (Unaohusu Matumizi bora na Salama ya Vifaa na mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini.

3)  Uendeshaji wa TOVUTI ya Taasisi

Kitengo kwa kushirikiana na Kitengo cha Habari na Uhusiano tunaendesha tovuti ya Taasisis kwa kuweka Taarifa na Picha Rasmi zinazohusu Taasisi na huduma zinazotolewa na Taasisi.

4) Usimamizi wa Mifumo na Miundombinu

Kitengo kinasimamia Upatikanaji wa Mifumo mbalimbali baadhi ni kama ifuatavyo:-

  • Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Wanafunzi na Ukusanyaji Mapato (OSIM)
  • Mfumo wa Uhasibu Serikalini (MUSE)
  • Mfumo wa Upangaji wa Bajeti ya Taasisi (PlanRep)
  • Mfumo wa Ununuzi (TANePS)
  • Mfumo wa Serikali wa Utumishi(HCMIS)
  • Mfumo wa Barua pepe za Serikali

5) Maabara ya Kompyuta

Kitengo pia kinasimamia utoaji wa Huduma ya Matumizi sahihi ya Maabara za Kompyuta (Computer Labs) ikiwemo ufundishaji pamoja na Mazoezi kwa Vitendo kwa Wanafunzi.

NB:Kwa huduma zote za TEHAMA chuoni usisite kuwasiliana na Kitengo kupitia barua pepe:  ict@dmi.ac.tz