Program za Shahada ya Uzamili

1.  Sifa za Kujiunga Shahada ya Uzamili katika Uchumi wa Usafirishaji na Logistiki (MSEL)

 Muundo wa Programu:

  • Mwenye Shahada ya Kwanza katika fani ya Usafirishaji/Ununuzi, Logistiki na Usimamizi wa Usafirishaji/ Shahada ya Kwanza katika fani ya Usafiri wa Majini, Uhandisi wa Bahari, Sayansi, Uhandisi, Usimamizi wa Biashara, Uchumi, Uhasibu na Hisabati/Takwimu mwenye GPA si chini ya 2.7; Au
  • Mwenye Stashahada ya Juu ya Usimamizi wa Usafirishaji/Usafirishaji/Bandari/Ununuzi, Usafirishaji na Ugavi/ Usafiri wa Baharini na Uhandisi wa Baharini mwenye GPA si chini ya 3.0; Au
  • Mwenye Shahada ya Kwanza ambayo haijainishwa GPA yake katika fani ya Logistiki na Usimamizi wa Usafirishaji/ Ugavi, Logistiki na Usimamizi wa Usafirishaji/ Shahada ya Kwanza katika fani ya Usafiri wa Baharini, Uhandisi wa Bahari, Sayansi, Uhandisi, Usimamizi wa Biashara, Uchumi, Uhasibu na Hisabati/Takwimu kwa kupata ufaulu nzuri.

Muda wa Kozi:

Muda wa kozi ni miaka (2) miaka ya masomo ambayo imepangwa katika mihula minne.

2.  Sifa za Kujiunga Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Usafirishaji (MTSM) Muundo wa Programu:

  • Mwenye Shahada ya Kwanza katika fani ya Usafirishaji/Ununuzi, Logistiki na Usimamizi wa Usafirishaji/ Shahada ya Kwanza katika fani ya Usafiri wa Majini, Uhandisi wa Bahari, Sayansi, Uhandisi, Usimamizi wa Biashara, Uchumi, Uhasibu na Hisabati/Takwimu mwenye GPA si chini ya 2.7; Au
  • Mwenye Stashahada ya Juu ya Usimamizi wa Usafirishaji/Usafirishaji/Bandari/Ununuzi, Usafirishaji na Ugavi/ Usafiri wa Baharini na Uhandisi wa Baharini mwenye GPA si chini ya 3.0; Au
  • Mwenye Shahada ya Kwanza ambayo haijainishwa GPA yake katika fani ya Logistiki na Usimamizi wa Usafirishaji/ Ugavi, Logistiki na Usimamizi wa Usafirishaji/ Shahada ya Kwanza katika fani ya Usafiri wa Baharini, Uhandisi wa Bahari, Sayansi, Uhandisi, Usimamizi wa Biashara, Uchumi, Uhasibu na Hisabati/Takwimu kwa kupata ufaulu nzuri.

Muda wa Kozi:

Muda wa kozi ni miaka (2) miaka ya masomo ambayo imepangwa katika mihula mine

3.  Shahada ya Uzamili ya Sheria za Bahari na Biashara za Kimataifa

Muundo wa Programu:

Shahada ya Uzamili katika Biashara za Kimataifa na Sheria za Bahari ni kozi ya miaka miwili yenye jumla ya moduli 17 zinazojumuisha moduli 14 za lazima na moduli 3 za kuchaguliwa. Mwanafunzi atakamilisha utafiti kwa kuwasilisha tasnifu katika muhula wa nne.

Sifa za Kujiunga:

Waombaji watatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza ya Sheria, Shahada ya Kwanza ya Benki/Biashara, Fedha, Usafirishaji na Logistiki, Usafirishaji na Ugavi, Teknolojia na Uhandisi wa Baharini na awe na GPA si chini ya 2.7; AU

Aliye na Diploma ya Juu ya Usafiri wa Baharini / Uhandisi wa Baharini na GPA si chini ya 3.0

4.  Shahada ya Uzamili Katika Usimamizi wa Uhandisi wa Bahari

Muundo wa Programu:

Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Uhandisi wa Majini ni kozi ya muda wa miezi 24 yenye jumla ya moduli 15 na moduli 4 za kuchaguliwa. Wanafunzi watahitajika kuhudhuria moduli 15 (pamoja na Utafiti) na moduli 1 ya kuchaguliwa. Moduli itafundishwa ndani ya muhula mmoja wa wiki 15 za kufundisha na wiki 2 kwa mtihani wa muhula wa chuo ili kufanya wiki 17. Muundo huu utafundishwa ndani ya mihula minne.

Sifa za Kujiunga:

Waombaji watahitajika kuwa na Shahada ya Kwanza ya Teknolojia ya Uhandisi wa Bahari, Uhandisi wa Mitambo, Uhandisi wa Umeme, Uhandisi wa Magari, Usanifu wa Majini na Ujenzi wa Meli, Uhandisi wa Pwani, Uhandisi wa Mafuta au Uhandisi wa Umeme na awe na GPA si chini ya 2.7 AU

Aliyehitimu Diploma ya Juu ya Teknolojia ya Uhandisi wa Bahari, Uhandisi Mitambo, Uhandisi wa Umeme, Uhandisi wa Magari au Uhandisi wa Umeme na awe na GPA si chini ya 3.0