NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI APONGEZA DMI KUSHIRIKI MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE

Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe.David Kihenzile (MB) Leo tarehe 08 ametembelea Banda la Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) wakati wa Maadhimisho ya kilele cha siku ya Wakulima kwenye maonesho yanayoendelea Kitaifa kwenye Viwanja vya Nzuguni -Dodoma.
Naibu Waziri amekipongeza Chuo kwa kushiriki maonesho hayo kwa kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu uhusiano uliopo baina ya maadhimisho ya Wakulima na Elimu na Mafunzo yanayotolewa Chuoni.
Maonesho ya Wakulima Nanenane yatahitimishwa rasmi tarehe 10/08/2024 baada ya kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 08/08
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe.David Kihenzile (MB) akizungumza na watumishi wa DMI alipotembelea banda kwenye maonesho ya wakulima nanenane.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe.David Kihenzile (MB) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la DMI kwenye maonesho ya wakulima nanenane.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe.David Kihenzile (MB) akipokea zawadi ya notebook kutoka kwa Msajili wa wanafunzi Rehema Juma alipotembelea banda la DMI kwenye maonesho ya wakulima nanenane.