“NAWAHAMASISHA UJUZI MLIOUPATA UTUMIKE KUFUATA SHERIA NA MIONGOZO KATIKA MATUMIZI SAHIHI YA TEHAMA". DKT. TUMAINI.

10 Mar, 2023
“NAWAHAMASISHA  UJUZI MLIOUPATA UTUMIKE KUFUATA SHERIA NA MIONGOZO KATIKA MATUMIZI SAHIHI  YA TEHAMA". DKT. TUMAINI.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar Es Salaam Dkt. Tumaini Gurumo amewasisitiza watumishi wa DMI kufanyia kazi mafunzo ya makosa ya kimatandao na matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA yaliyotolewa kwa kufuata sheria na miongozo iliyowekwa kwa maendeleo ya Taasisi na Serikali.

Hayo ameyazungumza leo alipokuwa akifunga mafunzo yaliyotolewa kwa watumishi yaliyoanza jana na kuongeza kuwa Serikali imeweka kipaumbele kwenye matumizi ya mifumo ya TEHAMA hivyo watumishi pia wanapaswa kujifunza zaidi ili kuendana na kasi ya Serikali.

Ameongeza kuwa Serikali imeweka sheria na miongozo ya matumizi ya mitandao na mifumo ya KITEHAMA, hivyo ili tuwe salama ni vyema kutumia ujuzi uliotolewa katika mafunzo hayo kwenye utendaji kazi wa kila siku.

Aidha amekipongeza kitengo cha TEHAMA na waataalamu kutoka e-Government na watumishi wote kwa ujumla kwa kushiriki mafunzo hayo ambayo yamelenga kuimarisha matumizi bora ya mifumo ya TEHAMA kwa Taasisi na Serikali kwa ujumla.

Leo watumishi wameweza kufundishwa maana ya udukuzi, aina zake, njia zinazopelekea kudukuliwa na mbinu za kuepuka udukuzi wa kimtandao.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar Es Salaam Dkt. Tumaini Gurumo akiwasisitiza watumishi kufanyia kazi mkafunzo waliyopewa kwa kufuata sheria na miongozo iliyowekwa ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar Es Salaam Dkt. Tumaini Gurumo  (katikati), Makamu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam,Utawala fedha na Mipango Dkt.Wilfred Kileo (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Raymond Chambua (kulia)  wakifuatilia hitimisho la mafunzo ya matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA.

Mtaalamu kutoa Mamlaka ya Serikali Mtandao akitoa mafunzo ya udukuzi kwa watumishi wa DMI.

Mwalimu wa masulala yasheria, Mwanasheria  Hiacinter  Rwechungura akishukuru kwa niaba ya wafanyakazi wa DMI kwa mafunzo yaliyotolewa, kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bw. Raymond Chambua.