Mwalimu, Injinia Miraji Mkwande kushoto, akiwasimamia wanafunzi wanaochukua masomo ya uinjinia wakati wa mafunzo kwa vitendo yaliyofanyika kwenye karakana ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI).
Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt. Tumaini Gurumo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliochaguliwa kwenda mafunzoni Nchini Korea kabla ya kuanza safari nje ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Wanafunzi wa Chuo cha Bahari wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo ya uokozi kwa kutumia Life Jacket
Wanafunzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam, Eric Ceaser na Wilfrida wakitoa elimu ya uokozi kwa kutumia life jacket kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisimiri iliyopo Meru , Arusha wakati Timu ya DMI ilipotembelea shuleni hapo.
Waziri wa Elimu na Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhamed akitoa mapendekezo ya kuanzishwa kwa tawi la chuo Zanzibar na kuongeza programu za utoaji elimu ya ukozi kwa jamii alipotembelea banda la DMI kwenye maonesho ya TVET, Arusha.
Kuwa taasisi bora katika mafunzo, utafiti na ushauri katika taaluma za baharini na zinazohusiana
Dira
Kutoa mafunzo ya hali ya juu yanayo endeshwa na mahitaji, utafiti na huduma za ushauri katika taaluma za baharini na taaluma zinazo husiana katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara na kwingineko