WOMESA WAENDESHA MAFUNZO JINSI YA KUFIKIA MALENGO KWA WANAFUNZI WA KIKE WA DMI

20 May, 2023
WOMESA WAENDESHA MAFUNZO JINSI YA KUFIKIA MALENGO KWA WANAFUNZI WA KIKE WA DMI

Umoja wa wanawake waliopo kwenye Sekta ya Bahari na Bandari (womesa) jana tarehe 19 wameendesha semina ya mafunzo kwenye ukumbi wa 6 uliopo Chuo cha Bhari Dar es Salaam iliyohusisha wanafunzi wa chuoni hapo kwa lengo la kuwasaidia kufikia malengo yao baada ya kuona changamoto ambazo watoto wa kike wamekuwa wakikutana nazo katika kufikia ndoto zao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo Makamu Mkuu wa Chuo Fedha, Utawala na Mipango Dkt.Johnson  Kileo alisema kuwa, watoto wa kike ni wa muhimu sana katika jamii kwakuwa taifa linategema sana mchango wao katika kuleta maendeleo, na kuongeza kuwa, hakuna mwanaume  aliyeweza kusimama bila kuwa na mwanamke hivyo ni muhimu kujiheshimu na kuweka jitihada katika masomo  yao pasipo kukata tamaa ili kufikia malengo yao.

Naye Bw. Julius Nguhula aliwasisitiza  wanafunzi kuacha tabia za kupenda alama  za bure na badala yake waweke jitihada katika masomo yao ili kupata alama halali zitakazowasaidia kuwa bora  na kupata utaalamu unaohitajika kwani jamii inahitaji wataalamu wenye weredi na watoto wakike wanaojitambua  katika kuleta maendeleo. 

Mshauri wa wanafunzi Injinia Regina Mbilinyi aliwataka wanfunzi kwa kike kuwa na ushirikiano baina yao wenyewe ili kujenga umoja kati yao na kuwa imara pamoja na kuacha tabia ya kutoa visingizio mbalimbali vinavyopelkea kukosa masomo na mitihani.

Naye mwanasaikolojia Ms. Fides Filbert aliwashauri wanafunzi nkutumia ofisi ya mshauri vyema ili kuepuka  msono wa mawazo utakaopelekea kushindwa kufikia ndoto zao.

Semina hiyo inatarajiwa kuwabadilisha wanafunzi wa kike wa chuo cha bahari dar es salaam kuwa na mtazamo chanya ambao utawasaidia katika kufikia malengo yao na kuifanya seka ya bahari  kuwa imara.

Mwenyekiti wa Chama cha wanawake waliopo kwenye Sekta ya Bahari na Bandari (WOMESA) Fortunata Kakwaya akitoa neno la utangulizi wa semina, kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Fedha Mipango na Utawala Dkt.Johnson Kileo.

Makamu Mkuu wa Chuo Fedha Mipango na Utawala Dkt.Johnson Kileo akifungua semina kwenye ukumbi wa Hall 6 uliopo Chuo cha Bahari Dar es Salaam.

Semina ikiendelea kutolewa kwa wanafunzi wa kike na wanawake waliopo kwenye sekta ya bahari na Bandari.

 

Picha ya pamoja baada ya semina kumalizika.