WATUMISHI WA DMI WATAKIWA KUWA MAKINI NA MAKOSA YA KIMTANDAO

09 Mar, 2023
WATUMISHI WA DMI WATAKIWA KUWA MAKINI NA MAKOSA YA KIMTANDAO

Makamu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam,Utawala fedha na Mipango Dkt.Wilfred Kileo amewataka watumishi wa DMI kufuatilia kwa umakini mafunzo ya makosa ya kimatandao (Cyber Crime) yanayotolewa na kitengo cha TEHAMA kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Serikali Mtandao (e-Government) ili kuiweka Taasisi na watumishi mahali salama.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyotolewa kwa watumishi wote leo kwenye ukumbi wa Chuo alisema, watumishi wanapaswa kutokuchukulia makosa ya kimatandao kwa urahisi kwa sababu kuna sheria zinazosimamia makosa hayo na ikitokea kuna uvunjifu mtumishi au Taasisi itapaswa kuwajibika.

Aidha ameongeza kuwa Mafunzo hayo yanatolewa ili kujenga uelewa wa pamoja wa namna ya kuweza kuzuia makosa ya kimtandao yasijitokeze hivyo ni muhimu kwao kufuatilia na kuelewa namna bora ya matumizi ya miundombinu ya TEHAMA yanayotumika Chuoni, kwani tunahitaji mabadiliko ya kiteknolojia lakini pia tunahitajika kufuata sheria.

Aliongeza kuwa haifai mtumishi kuchukulia wepesi anapopotelewa na kifaa cha TEHAMA kwani tupo katika kipindi kigumu ambacho teknolojia inakua kwa kasi na Serikali inaitazama mifumo ya kitehama kwa namna ya tofauti.

Kwa upande wake mwenyekiti wa maandalizi ya andiko la Sera ya TEHAMA ya DMI (DMI ICT POLICY) Jonnese Lugoye Lugoye amesema kuwa ni vyema kuwatumia wataalamu wa TEHAMA pale inapohitajika ili kufanya matumizi sahihi ya miundombinu ya TEHAMA ikiwa ni pamoja na kuitunza.

Mafunzo haya natarajiwa kuendesha kwa siku mbili yaani leo na kesho ambapo kwa siku ya leo watumishi waliweza kujifunza juu ya Sera ya TEHAMA ya DMI (DMI ICT POLICY),Matumizi sahihi ya miundombinu ya TEHAMA,Utendaji kazi wa Mamalaka ya Serikali mtandao (e_Gavernment),Sera za ulinzi wa TEHAMA za DMI (dmi ict security policy) na Utoaji huduma wa TEHAMA kwa kufuata miongozo.

Afisa TEHAMA mwandamizi , Siganike Baruti akitoa mafunzo ju ya matumizi sahihi ya miundombinu ya TEHAMA.

Mwenyekiti wa maandalizi ya andiko la Sera ya TEHAMA ya DMI (DMI ICT POLICY) Jonnese Lugoye akizungumza juu ya umuhimu wa kutambua matumizi sahihi ya miundombinu ya TEHAMA.

 


 

Mwenyekiti wa maandalizi ya andiko la Sera ya TEHAMA ya DMI (DMI ICT POLICY) Jonnese Lugoye akiwasilisha mafunzo juu ya DMI  ICT POLICY

 

Afisa TEHAMA  Mwandamizi, Nolelo Ng'ingu akiwasilisha mafunzo juu ya Sera za ulinzi wa TEHAMA za DMI (DMI ICT security policy)

Watumishi wakifuatilia uwasilishwaji wa mafunzo

Watumishi wakifuatilia uwasilishwaji wa mafunzo

Watumishi wakifuatilia uwasilishwaji wa mafunzo

Watumishi wakifuatilia uwasilishwaji wa mafunzo.

Afisa TEHAMA mwandamizi , Siganike Baruti akitoa mafunzo ju ya matumizi sahihi ya miundombinu ya TEHAMA.

Afisa TEHAMA Liberius Kalabamu akiwasilisha mada ya Utoaji huduma wa TEHAMA kwa kufuata miongozo.

Mtumishi wa DMI akichangia mada mara baada ya wasilisho kutoka kwa muwezeshaji.

Yasinta Mwalimu DMI akichangia mada baada ya wasilisho la mafunzo kutoka kwa muwezeshaji.

Viorine Mamku, mwalimu wa Kompyuta DMI akiwasilisha  mada ya utendaji kazi wa mamlaka ya serikai mtandao

Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Veronica Sudayi akichangia mada baada ya wasilisho la mafunzo kutoka kwa muwezeshaji.

Mshauri wa wanafunzi, Injinia Regina Mbilinyi  akichangia mada baada ya wasilisho la mafunzo kutoka kwa muwezeshaji.