WATUMISHI TUDUMISHE USHIRIKIANO KAZINI- DKT TUMAINI

18 Aug, 2023
WATUMISHI TUDUMISHE USHIRIKIANO KAZINI- DKT TUMAINI

Watumishi wa Chuo Cha Bahari Dar es salaam (DMI) wamehimizwa kudumisha ushirikiano ili waweze kutekeleza majukumu ya Taasisi kupitia bajeti iliyopangwa kwa lengo la kuongeza nafasi ya kuendelea kuzitangaza zaidi fursa zilizopo Chuoni kwa jamii.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa DMI Dkt.Tumaini Gurumo (Mkuu wa Chuo) wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Foundation.

Mwenyekiti Dkt.Tumaini Gurumo amesema kuwa Chuo kinaendelea kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi ili kuongeza tija ya utekelezaji wa majukumu kwa kila Mtumishi, Hivyo ni muhimu kuwajibika katika kukitangaza Chuo kupitia fursa zilizopo.

Aidha, Uongozi wa chama cha wafanyakazi RAAWU wamepongeza menejimenti na uongozi wa Chuo Kwa jitihada wanazoendelea kuchukua kuhakikisha wanaboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wote.

 

Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa DMI Dkt.Tumaini Gurumo (Mkuu wa Chuo) wa katikati, akizungumza na watumishi wakati wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi .