WANAWAKE WA DMI WAHIMIZWA KUHAMASISHA MABINTI MASOMO YA SAYANSI

09 Mar, 2024
WANAWAKE WA DMI WAHIMIZWA KUHAMASISHA MABINTI MASOMO YA SAYANSI

Katika kuelekea kilele cha siku ya wanawake duniani Machi 8 yenye kauli mbiu ya “Wekeza kwa wanawake ili kuharakisha maendeleo ya Taifa pamoja na ustawi wa jamii”, leo Wanawake wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) wametakiwa kuhamasisha mabinti kujiunga DMI kwenye fani za masomo ya sayansi na uhandisi ili kuongeza idadi ya wanawake kwenye Taaluma hizo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa semina ya wanawake wa DMI iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere Foundation, Mkurugenzi wa Taaluma Dkt. Werneld Ngongi amesema, taaluma ya sayansi na uhandisi ina vijana wa kike wachache na fursa zipo wazi kwao hivyo ni vyema kuhamasishwa.

Aidha amepongeza umoja wa wanawake uliopo ndani ya Chuo na Kupongeza utayari wa Mkuu wa Chuo katika kuwezesha mafunzo ambayo yametolewa kwa wanawake wote wa DMI kwa lengo la kuwaimarisha zaidi katika kukuza ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla.

“Nimpongeze Mkuu wa Chuo kwa kuwezesha mafunzo na Idara ya Rasilimali watu kwa kuratibu mafunzo haya muhimu ambayo hayajawahi kufanyika tangu kuanza kwa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hapa Chuoni, sisi wanaume tupo nyuma yenu na tunatambua mchango wenu katika ukuaji wa jamii na taifa hivyo niwaombe mtumie muda wenu vizuri kujifunza katika semina hii na kuiishi kauli mbiu ya mwaka huu” alisema Dkt. Ngongi

Wanawake wa DMI wamepata semina kuhusu living life balance kutoka kwa mwezeshaji Aunt Sadaka Gandi na kujumuika Kwa kupata chakula cha pamoja.

Mkurugenzi wa Taaluma Dkt. Werneld Ngongi akizungumza na wanawake wa DMI kwenye semina iliyoandaliwa na ofisi ya rasilimali watu.

Mwezeshaji Aunt Sadaka Gandi  akizungumza na wanawake kuhusu living life balance kwa ustawi binafsi,jamii na taifa kwa ujumla katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere foundation.

 

 

 

 

 

Picha ya pamoja kati ya mwezeshaji Aunt Sadaka Gandi (katikakati), kulia ni Meneja Rasilimali watu Christine Nderumaki na Kushoto ni Mhandisi Regina Mbilinyi na wanawake wa DMI mara baada ya hitimisho la semina fupi.