WANAFUNZI WENGINE WATANO KUSHIRIKI MAFUNZO KWA VITENDO MELINI KOREA KUSINI.

Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimefanikiwa kuwapeleka wanafunzi watano kufanya mafunzo kwa vitendo melini katika Chuo cha Bahari cha Korea KIMFT (Korea Institute of Maritime and Fisheries Technology) ikiwa ni matunda ya ushirikiano baina ya Chuo hiki na KIMFT unaolenga kubadilishana uzoefu wa Mafunzo yanayohusu masuala ya Bahari.
Mkuu wa Chuo cha Bahari Dkt. Tumaini Gurumo akiwaaga Wanafunzi hao leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo, amewataka kuzingatia nidhamu, heshima, na juhudi katika Mafunzo pamoja na kutoacha asili ya kitanzania ili kuleta sifa Kwa Nchi na Chuo kwa ujumla.
Wanafunzi wanatarajia kuondoka nchini leo kwenda Korea kwa ajili ya mafunzo hayo ambayo yanatarajiwa kuchukua muda wa miezi mitatu.
Mkuu wa Chuo cha Bahari Dkt. Tumaini Gurumo akizungumza na wanafunzi wanaotarajiwa kwenda Chuo cha Bahari na Uvuvi cha Korea y Kusini KIMFT.
Mkuu wa Chuo cha Bahari Dkt. Tumaini Gurumo akizungumza na wanafunzi wanaotarajiwa kwenda Chuo cha Bahari na Uvuvi cha Korea y Kusini KIMFT.
Wanafunzi watano wanaotarajiwa kujiunga na mafunzo kwa vitendo Korea Kusini