WAKUFUNZI WA DMI WAJENGEWA UWEZO KUHUSU SHUGHULI ZA BOMBA LA MAFUTA LA AFRIKA MASHARIKI

26 Mar, 2025
WAKUFUNZI WA DMI WAJENGEWA UWEZO KUHUSU SHUGHULI ZA BOMBA LA MAFUTA LA AFRIKA MASHARIKI

Wakufunzi na Wahadhiri wa Chuo Cha Bahari Dar es Salaam wamepatiwa Mafunzo kuhusu Train the Trainer kwa lengo la kuwajengea uwezo na Uelewa wa Shughuli za Uhandisi,Manunuzi, ugavi,Usambazaji na Lojistiki katika Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki ( East African Crude Oil Pipeline,EACOP).



Mafunzo hayo yanalenga kunufaisha Wakufunzi na Wahadhiri wa DMI kwenye eneo la Utoaji Elimu na Mafunzo na kubaini fursa zinazoletwa na Mradi wa bomba la Mafuta la Afrika Mashariki (EACOP). Aidha Mafunzo hayo pia  ni sehemu ya kutimiza majukumu ya Mkataba Hodhi wa Serikali (Host Government Agreement).



Ni jukumu muhimu Kwa Mradi na Wakandarasi wake,kama inavyotakiwa na local content katika kuboresha Elimu na mafunzo yanayotolewa kwenye Vyuo na Taasisi za Elimu na Mafunzo nchini Tanzania.

Mafunzo hayo yamefanyikia tarehe 25/03/2025 kwenye ukumbi namba 2 wa Chuo Cha Bahari ukiwa umeandaliwa na Mkandarasi wa Bomba la Mafuta, Worley - EACOP