WAJUMBE WA BODI YA DMI WATEMBELEA MTAMBO WA KISASA WA KUFUNDISHIA CRANE SIMULATOR

10 Nov, 2023
WAJUMBE WA BODI YA DMI WATEMBELEA MTAMBO WA KISASA WA KUFUNDISHIA CRANE SIMULATOR

Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) wamefanya ziara ya kuona utendaji kazi wa mtambo wa kisasa wa kufundishia CRANE SIMULATOR wenye thamani ya Bilioni 2.5 unaolenga kuongeza tija ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa kozi za usafirishaji na lojistiki.

Wajumbe wa Bodi wamepongeza hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuwezesha chuo kupata mtambo huo utakao zalisha wataalamu watakaoendana na teknolojia katika kukidhi soko la ajira.

 Mtambo huu utatumika kuzalisha wataalamu watakaofanya kazi maeneo ya Bandari, Viwandani na Migodini.

Pia, Chuo kinakaribisha maombi ya watu binafsi, mashirika na kampuni watakaohitaji  kupata huduma ya mafunzo ya namna ya kuendesha mitambo hii ya kisasa ya toleo la Mwaka 2022 kwaajili ya kuongeza ufanisi mahala pa kazi.

Ziara hii imefanyika leo tarehe 10/11/2023 katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI).