WAHITIMU 1326 WATUNUKIWA VYETI MAHAFLI YA 19 DMI

04 Dec, 2023
WAHITIMU 1326 WATUNUKIWA VYETI MAHAFLI YA 19 DMI

Mahafali ya 19 Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI) ambapo jumla ya Wanafunzi 1326 wamehudhurishwa na Naibu Waziri wa UChukuzi Mhe.David Kihenzile tarehe 30/11/2023

Miongoni mwao wanafunzi 9 ni wa Shahada ya Uzamili, 241 wa Shahada, 192 wa Stashahada , 323 wa Astashahada , 532 wa Astashahada ya Awali pamoja na wanafunzi wapatao 29 wa vyeti vya umahiri (CoC).

Katika jumla ya Wanafunzi 1326, Wanafunzi wakike ni 403 na Wanaume ni 923 na Wanafunzi kutoka nje ya Tanzania ni 15.

Chuo Cha Bahari Dar es salaam (DMI)ni kimoja kati ya vyuo vinne (4) vya kikanda barani Afrika; na kinafanyiwa ukaguzi na shirika la kimataifa linalosimamia masuala ya bahari (IMO) kila baada ya miaka mitano ili kuhakikisha ubora na kutambulika kimataifa kwa kozi za ubaharia na kozi za umahiri kwa maafisa wa meli.

Aidha, Chuo kina cheti cha Ubora cha ISO 9001:2015.

Kozi za kitaaluma zinazotolewa na chuo zina ithibati ya NACTVET.

Chuo kinatoa kozi ndefu yaani kuanzia Cheti mpaka kozi za shahada ya Uzamili, na fupi yaani (short course) pamoja na kozi za Cheti Cha umahiri (Certificate of Competence).

Katika kupanua wigo wa fursa za ajira Chuo kimeendelea kufanya utafiti wa uhitaji wa rasilimali watu na kuandaa mitaala mipya na kurekebisha iliyopo ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira katika sekta ya bahari.

Aidha, kupitia kitengo chake cha ‘DMI Crewing Agency’ DMI imeendelea kushiriki kwa dhati katika kutekeleza adhma ya Serikali yetu ya kuongeza ajira kwa vijana kwa kuwatafutia kazi ndani na nje ya Nchi.