WADAU WAKUTANA KUTOA MAONI KUHUSU MPANGO WA DMI WA KUKABILINA NA MAJANGA

24 Oct, 2023
WADAU WAKUTANA KUTOA MAONI KUHUSU MPANGO WA DMI WA KUKABILINA NA MAJANGA

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es salaam Dkt.Tumaini Gurumo  amewakaribisha na kuwaomba kushiriki kikamilifu wadau walioshiriki warsha ya kutoa maoni na mapendekezo ya mpango wa chuo cha bahari wa kukabiliana na majanga ulioandaliwa kwa lengo la kujiandaa kukabiliana na majanga pindi yatakapotokea.

Akiwakaribisha wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Bahari Dkt.Tumaini amesema kuwa, ni vyema kuandaa miundombinu ya kukabiliana na majanga ili pindi yanapotokea iwe rahisi  kuepuka na kukabiliana na madhara.

“Aliyejiaandaa ni bora kuliko asiyejiandaa”Alisema Dkt.Tumaini

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Fedha, Utawala na Mipango Dkt.Lucas Mwisila akifunga warsha hiyo amesema kuwa, Chuo kinapenda kuhusisha wadau katika njanja mbalimbali ili kupata maarifa na uzoefu tofauti tofauti na kwamba maoni na mapendekezo yaliyotolewa yatafanyiwa kazi katika kuboresha mpango huo utakao tumika hata kwa vizazi vijavyo.

Taasisi kutoka maeneo mbalimbali kama TASAC, TCRA, TTCL, SUMA JKT, Uhamiaji, Hazina, Ziamamoto, REDCROSS, EGA, Polisi Ilala, MARINE POLICE na CRDB Bank wameshiriki kutoa maoni yao katika kuboresha mpango wa kukabiliana na majanga wa DMI.

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es salaam Dkt.Tumaini Gurumo akitoa historia fupi ya chuo na kuwakaribisha wadau  kutoa maoni na mapendekezo ya mpango wa kukabiliana na majanga 

Wadau wakiwa kwenye kundi la majadiliano ya mapendekezo ya mpango wa kukabiliana na majanga 

Wadau wakiwa kwenye kundi la majadiliano ya mapendekezo ya mpango wa kukabiliana na majanga 

Wadau wakiwa kwenye kundi la majadiliano ya mapendekezo ya mpango wa kukabiliana na majanga 

Makamu Mkuu wa Chuo Fedha, Utawala na Mipango Dkt.Lucas Mwisila akifunga warsha na kuwashukuru wadau.