WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUTOA MAONI JUU YA MITAALA.

24 Aug, 2023
WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUTOA MAONI JUU YA MITAALA.

Wadau Elimu ya juu nchini leo wamekutana katika  Chuo cha Bahari Dar es Salaam kwenye ukumbi wa chuo (Hall 2) kutoa maoni yao kuhusu  mitaala  inayohuishwa na inayotarajiwa kutengenezwa na Chuo ili kuendana na mahitaji ya soko na matakwa ya sheria zinazosimamia mafunzo ya Ufundi ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).

Akifungua majadiliano hayo, Mkuu wa Chuo cha Bahari cha Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo amesema kuwa, upo umuhimu wa  kuboresha mitaala ya Chuo ili kuendana na wakati, uhitaji wa soko na mabadiiko ya teknolojia.

“Naomba tujadiliane vizuri  na tuweke maoni mbalimbali ili tupate mitaala itakayosaidia kutatua changamoto zilizopo katika sekta hii ya usafirishaji kwa njia ya maji na  kuiwezesha jamii na Taifa kwa ujumla  kunufaika na fursa zitokanazo na Uchumi wa Buluu” Alisema Dkt. Tumaini.