UONGOZI WA SERIKALI YA WANAFUNZI DMI WAPIGWA MSASA

25 Aug, 2023
UONGOZI WA SERIKALI YA WANAFUNZI DMI WAPIGWA MSASA

Chuo cha Bahari Dar es Salaam leo kupitia Ofisi ya mshauri wa wanafunzi  kimetoa  semina kwa viongozi wapya wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Bahari kwa Lengo la kuimarisha Uongozi  huo ili kuweza kutatua changamoto za wanafunzi wakiwa kama wawakilishi wao.

Makamu Mkuu wa Chuo Cha Bahari Dar es salaam Fedha, Utawala na Mipango Dkt Lukas Mwisila akifungua semina hiyo amewasisitiza viongozi wa wanafunzi kufatilia kwa makini taarifa mbalinbali za wanafunzi  wenzao ili kuwaepusha na  matatizo mbalimbali yanayoweza kujitokeza.

Pia,Viongozi hao wamehamasishwa kuwa na maadili na nidhamu katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuimarisha mawasiliano ili kuepusha migogoro baina yao na wanafunzi,  kutokua wakatili , kuwa na nidhamu ya fedha  katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kusisitizwa kujenga afya ya akili ili wawe tayali kisaikolojia kutatua changamoto za wanafunzi.