UJUMBE KUTOKA WORD MARITIME UNIVERSITY-SWEDEN WATEMBELEA DMI

19 Apr, 2024
UJUMBE KUTOKA WORD MARITIME UNIVERSITY-SWEDEN WATEMBELEA DMI

Ujumbe kutoka World Maritime University (WMU) umetembelea Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kwa lengo la kuona maendeleo ya utendaji kazi wa Chuo, pia kufuatilia maendeleo ya wataaluma waliowahi kusoma katika Chuo hicho akiwemu Mkuu wa Chuo cha Bahari (DMI) Dkt.Tumaini Gurumo.

Akizungumza kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo baada ya kuupokea ugeni huo Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam amesema kuwa ujio wa ujumbe huo  unaonesha mwanzo mzuri wa kujenga mahusiano ya kitaaluma utakaolenga kuongeza ufanisi wa rasilimali watu wa tasnia ya Bahari.

“Tumefurahi sana kuupokea ugeni huu, tunaona nuru mpya ya kuimarisha mashirikiano na WMU hususani katika kipindi hiki ambacho Chuo kinaendelea kukua kwa kasi” Alisema Dkt.Tumaini

Makamu wa Rais wa Masuala ya Taaluma kutoka World Maritime University Profesa Dk.Jens-Uwe Schroder-Hinrichs akizungumza na menejimenti ya Chuo amesema amefurahi kufika na kuona uhalisia wa maendeleo ya Chuo hususani mwamko wa wanafunzi wanaosoma masomo ya ubaharia ukilinganisha na Nchi za Ulaya.

Pia, Profesa Dkt. Anish Hebbar kutoka WMU amesema wamefurahi kufika Chuoni na kukuta kiongozi Mwanamke ambaye aliwahi kuwa mwanafunzi wao kipindi fulani. Kwao imekua ziara yenye tija katika kubadilishana uzoefu.

Wageni hao walipata fursa ya kutembelea miundombinu mbalimbali ya mafunzo kwa vitendo iliyopo Chuoni na kukutana na wahitimu waliowahi kusoma WMU, yaani Alumni ikiwa ni sehemu ya kufuatilia maendeleo yao na kuona namna wanavyotumia taaluma zao.

World Maritime University ni Taasisi iliyopo chini ya International Maritime Organization (IMO) inayojihusisha na kujengea uwezo    taasisi za bahari zilizopo katika nchi zinazoendelea.

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo akimkabidhi zawadi Profesa Dkt. Anish Hebbar kutoka WMU.

 

Ujumbe kutoka  WMU wakizungumza na Menejimenti ya Chuo cha Bahari kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo.

Ujumbe kutoka WMU wakipata maelezo mafupi juu ya uendeshaji wa kituo cha mitihani ya lugha ya kiingereza kwa mabaharia (English Marlins Test Centre) kilichopo Chuoni.

Mtaalamu wa Mtambo wa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wanaosoma kozi za usafirishaji Mhadhiri msaidizi Bw.Chesco Komba akielezea utendaji kazi wa mtambo huo (Crane Simulator) mara Ujumbe kutoka WMU ulipofika kutembelea eneo hilo.

Ujumbe kutoka WMU ulipotembelea kwenye chumba kilichofungwa mtambo wa Live Radar unaotumika kufundishia wanafunzi.

Mhandisi Gregory Mella akitoa maelezo kwa  ujumbe kutoka WMU walipotembelea kwenye chumba cha mtambo maalumu wa Engine Simulator kwaajili ya mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma Uhandisi wa Meli.

Mhandisi Gregory Mella akitoa maelezo kwa Ujumbe kutoka WMU walipotembelea kwenye chumba cha mtambo maalumu wa Engine Simulator unaotumika kwaajili ya mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma Uhandisi wa Meli.

Picha ya Pamoja baina ya Ujumbe kutoka WMU na Menejimenti ya DMI

Picha ya pamoja na Alumni wa WMU