MAFUNZO YA UANDAAJI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI KUPITIA MFUMO WA PLANREP

24 Aug, 2022
MAFUNZO YA UANDAAJI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI KUPITIA MFUMO WA PLANREP

Maafisa bajeti wapatao 17 kutoka Idara na Vitengo mbalimbali katika chuo cha bahari Dar es Saalam wapatiwa mafunzo ya namna ya kuandaa na kutekeleza bajeti kwa kutumia Mfumo wa PLANREP ambao umeunganishwa na mfumo wa malipo wa MUSE.

Kaimu Mkuu wa Chuo, Dkt. Wilfred J. Kileo (Aliyesimama) akitoa neno la ufunguzi

Kaimu Mkuu wa Chuo, Dkt. Wilfred Johnson Kileo, akiwa anafungua mafunzo hayo, aliwataka Maafisa bajeti kufuatilia kwa makini mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo katika masuala ya kuandaa na kutekeleza bajeti ili kuhakikisha shughuli za chuo zinatekelezwa na kukakamilika kulingana na mipango iliyojiwekea katika mwaka husika.

Kaimu Mkuu wa Chuo, Dkt. Wilfred J. Kileo (Katikati) katika picha ya pamoja na Wawezeshaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina

 

Dkt. Johson ametoa wito kwa maafisa bajeti kushirikiana na kusaidiana katika kutekeleza bajeti ili kufanikisha utekelezaji wa shughuli za taasisi ili taasisi iweze kusonga mbele.

Wawezeshaji wa mafunzo kutoka ofisi ya Msajili wa Hazina wakiteta jambo, Ndg. Emilian Bakuza, Afisa Usimamizi wa Fedha (Kushoto) na Ndg.Castory Mwageni, Afisa Usimamizi wa Fedha (Kulia)

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Kitengo cha Mipango na Maendeleo katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kwa kushirikisha wataalam kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina yanafanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 22 – 27/08/2022 katika Ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii – Dar es Salaam.

 

Timu ya Maafisa bajeti kutoka Idara na Vitengo mbalimbali wakiwa darasani