UONGOZI WA INTERNATIONAL MARITIME ORGANIZATION(IMO) WATEMBELEA DMI KUONA MAENDELEO YA UTENDAJI KAZI.

23 Mar, 2023
UONGOZI WA INTERNATIONAL MARITIME ORGANIZATION(IMO) WATEMBELEA DMI KUONA MAENDELEO YA UTENDAJI KAZI.Uongozi wa IMO ukiongozwa na Chief injinia Milhar Fauzudeen, William Azumo , pamoja na Kaptaini Dave Ngui Muli.umefanya ziara katika Chuo cha Bahari Dar Es Salaam(DMI) kwa lengo la kuangalia maendeleo ya utendaji kazi wa kitaaluma wa Chuo.

Akizungumza wakati wa kikao kifupi kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo, Kaimu Mkuu wa chuo Dkt.Tumaini Gurumo amesema chuo kimepewa mamlaka ya kutoa elimu inayohusiana na mambo ya Bahari katika Ngazi ya Cheti, Astashahada, Stashada na shahada ya uzamili, hivyo kinahitaji kuongeza miundombinu bora ili kufanya kiweze kutoa mafunzo kwa upana zaidi.

Chief engineer Milhar Fauzudeen amezungumza kuwa Chuo kinatakiwa kiongeze miundombinu ili kuweza kutoa mafunzo kwa ustadi zaidi, na kushauri uongozi wa Chuo kuongeza ushirikiano na Vyuo vya nje vinanvyo toa mafunzo ya Ubaharia ili kujifunza zaidi.

Ofisa William Azumo pamoja na kukipongeza Chuo kwa kufunga mtambo wa kisasa kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi, pia ameshauri kuwa ni vyema chuo kuweka hati (documents) mbalimbali kutoka IMO katika maktaba yake kwaajili ya rejea(reference) kwa wanafunzi.

Katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo wameweza kulijadiliwa ajenda mbali mbali ambazo zinalenga kuleta maendeleo katika chuo cha DMI katika Nyanja za Taaluma.

IMO ni Taasisi inayosimamia shughuli zote za Bahari duniani ikiwamo mazingira, usalama wa vyombo vya majini na kusimamia Vyuo vinavyotoa mafunzo ya masuala ya Bahari kuhakikisha vimekidhi vigezo stahiki.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es salaama DMI Dkt.Tumaini Gurumo akielezea elimu inayotolewa na Chuo kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo na viongozi kutoka IMO.

Chief injinia Milhar Fauzudeen kutoka IMO akitoa maoni yake ya uboreshaji wa miundombinu ya chuo ili elimu inayotolewa iweze kufika mbali zaidi.

Wajumbe wa Menejimenti wakifatilia majadiliano kuhusu uboreshaji wa Chuo cha Bahari DMI 

Wajumbe wa Menejimenti wakifatilia majadiliano kuhusu uboreshaji wa Chuo cha Bahari DMI 

 

Injinia Mlay akielezea utendaji kazi wa Simulator na namna unavyosaidia kwenye ufundishaji wa wanafunzi kwa viongozi wa IMO na DMI

Wajumbe wa Menejimenti wakifatilia majadiliano kuhusu uboreshaji wa Chuo cha Bahari DMI 

Picha ya pamoja ya Viongozi kutoka IMO na DMI mara baada ya kumaliza ziara chuoni hapo.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es salaama DMI Dkt.Tumaini Gurumo akimshukuru kiongozi kutoka IMO, Chief injinia Milhar Fauzudeen kwa kutembelea chuoni.