WATUMISHI WA TEMESA WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA BAADA YA MAFUNZO WANAYOPATIWA KATIKA CHUO CHA DMI
Naibu katibu mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Ludovick Nduhiye amewataka watumishi wa TEMESA wanaojiunga na mafunzo katika chuo cha DMI kusoma kwa weredi na kuongeza maarifa ili kuboresha ufanisi wa kazi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi wanaotumia vivuko.
Naibu katibu Mkuu Ameyazungumza hayo kwenye hafla fupi ya ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi 43 wa vivuko vinavyosimamiwa na TEMESA kote nchini iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo cha DMI, mafunzo hayo yamelenga kuongeza sifa za elimu kwa watumishi na kuongeza motisha kwao hali itakayopeleka kutolewa kwa huduma bora za vivuko.
Aidha Naibu katibu Mkuu amewataka watumishi hao mara baada ya kumaliza mafunzo hayo kuhakikisha wanashughulikia malalamiko ya wananchi,usalama wa wananchi na utunzaji mzuri wa vyombo wanavyoviendesha kwani serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya vivuko.
Naibu katibu Mkuu amekipongeza chuo cha DMI kwa kuendelea kutoa mafunzo katika kozi mbalimbali na kuifanya Nchi kuzalisha wataaalamu wengi kwenye Sekta ya Bahari hasa ukizingitia ndio chuo pekee kinachotoa mafunzo hayo.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Bahari (DMI) Dkt.Tumaini Gurumo amesema chuo kinayofuraha kuwapokea watumishi hao na kuongeza kuwa uchaguzi walioufanya TEMESA ni bora zaidi kwani DMI ni mahalai sahihi kwa mafunzo waliyolenga kuwapatia watumishi wao na kuwataka watumishi hao kuwa mabalozi wazuri mara baada ya kuhitimu mafunzo yao.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa ushirikiano uliopo wa elimu, ushauri wa kitaalamu wa ujenzi wa vivuko baina ya TEMESA na DMI unazidi kuimarika siku kwa siku hivyo kuendelea kuboresha utoaji wa huduma bora za vivuko vinavyosimamiwa na TEMESA nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TEMESA Lazaro Kilahala amesema watumishi 43 wanatoka katika vituo 16 kati ya 22 vinavyoendeshwa na Wakala ambapo, watumishi 9 watapata mafunzo ya awali ya lazima (mandatory course), mafunzo ya wasaidizi wa manahodha (rating Navigation Deck) watumishi 06, mafunzo ya mafundi sanifu (rating engine course) mtumishi 1, manahodha daraja la IV (COC Class IV Deck) watumishi 10 na uhuishaji vyeti (Revalidation Courses) watumishi 17 na jumla ya Tsh. 135 Milion zitatumika ikijumuisha ada pamoja na gharama za ushiriki.
Naibu katibu mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Ludovick Nduhiye akizungumza na watumishi wa TEMESA wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwenye viwanja vya DMI.
Naibu katibu mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Ludovick Nduhiye akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa Chuo cha DMI Dkt.Tumaini Gurumo na viongozi wengine kueleka eneo la ufunguzi wa mafunzo ya watumishi wa TEMESA
Baadhi ya watumishi wa TEMESA
Mkuu wa Chuo cha Bahari (DMI) Dkt.Tumaini Gurumo akiwapokea watumishi wa TEMESA waliofika kupata mafunzo.
Mkurugenzi Mkuu wa TEMESA Lazaro Kilahala akizungumza wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa mafunzo
Picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mafunzo