MAAFISA NA MAOFISA KUTOKA JESHI LA WANAMAJI WA TANZANIA NA NAMIBIA WATEMBELEA CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM (DMI)

13 May, 2026
MAAFISA NA MAOFISA KUTOKA JESHI LA WANAMAJI WA TANZANIA NA NAMIBIA WATEMBELEA CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM (DMI)

Maafisa na Askari kutoka Jeshi la Wanamaji wa Tanzania na Namibia wametembelea chuo cha Bahari Dar es Salaam(DMI) kwa lengo la kujifunza huduma za mafunzo zinazotolewa na chuo  hiko katika kuandaa wataalamu wa sekta ya bahari.

 Kamanda wa Jeshi la Majini Tanzania   Rear Admiral Hassanalieleza kuwa Tanzania ni mwanachama wa SADC, ambayo inajumuisha pia mataifa ya ukanda wa bahari ikiwemo Namibia. Alibainisha kuwa kupitia Kamati ya Masuala ya Bahari ya SADC nchi wanachama hushirikiana katika kubadilishana taarifa, mafunzo na kuimarisha uwezo katika sekta ya bahari. 


“Alieleza kuwa ameona umuhimu wa kukutanisha DMI na Kamanda wa Jeshi la Majini Namibia ili kupata fursa ya kufahamiana na kujuzana kuhusu shughuli za mafunzo” alisema Hassan.


Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Majini Namibia Rear Admiral Gonteb alikielezea kuwa DMI ni taasisi bora inayozalisha wataalamu wenye viwango na kutoa kozi za STCW. Alieleza kuvutiwa na ubora wa mafunzo, uwepo wa programu hadi ngazi ya Shahada ya Uzamili, pamoja na miundombinu ya mafunzo kwa vitendo.

Aidha, alisema kuwa katika uzoefu wake wa kutembelea taasisi mbalimbali, hajawahi kuona chuo chenye muunganiko mpana wa fani za bahari kama DMI, hususan kwa kuunganisha mafunzo ya STCW na ufundi stadi.

“Aliongeza kuwa wamejifunza mengi na wana matarajio ya kuendelea kujifunza zaidi, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kushirikiana katika maeneo ya mafunzo kupitia taasisi zao.” Alisema Gonteb


Kwa upande wake  Mkuu wa Chuo, Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Prof. Wilfred Kileo, aliwasilisha taarifa kuhusu shughuli za chuo. Alisema chuo kina ithibati za kitaifa na kimataifa pamoja na programu mbalimbali kuanzia ngazi ya cheti hadi Shahada ya Uzamili huku akibainisha mchango wa DMI katika kukuza rasilimali watu katika sekta ya bahari.


Maafisa na Askari hao pia walipata fursa ya kutembelea miundombinu ya mafunzo kwa vitendo chuoni hapo. 
DMI inaendelea kujiimarisha katika kutoa elimu yenye ubora kwenye sekta ya bahari kwa kuhudumia na kudahili wanafunzi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Oman,Uturuki, Namibia,Kenya, Kongo