MAOFISA KUTOKA IDARA NA VITENGO VYA DMI WAPATIWA MAFUNZO YA MENEJIMENTI UDHIBITI UBORA

29 Dec, 2022
MAOFISA KUTOKA IDARA NA VITENGO VYA DMI WAPATIWA MAFUNZO YA MENEJIMENTI UDHIBITI UBORA

Maafisa kutoka idara na vitengo mbalimbali wa  Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) leo wamepatiwa mafunzo ya uelewa wa pamoja juu ya udhibiti  ubora wa mfumo wa menejimenti (Quality Management System ISO 9001-2015) kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa utoaji huduma bora kwa wateja.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Foundation Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na Tafiti Dk.Lucas Mwisila amewasihi maofisa hao kuwafatilia kwa makini mafunzo hayo ili kuwawezesha kuboresha utendaji kazi kwenye maeneo yao na hatimaye kufikia malengo ya Taasisi.

Leo tarehe 29 maofisa wamefanikiwa kujifunza juu ya maana ya ISO, udhibiti ubora wa menejimenti namna inavyofanya kazi, faida zake, kanuni, malengo yake, dhana za msingi zinazotumika na PDCA Cycle(Plan, Do,Check and Act).

Mafunzo haya yameandaliwa na kuratibiwa na kitengo cha Uthibiti Ubora cha Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI )ambapo yanafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 29-30/12/2022 kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS)

Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na Tafiti Dk.Lucas Mwisila  akifungua mafunzo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyelele Foundation

Wataalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kushoto ni Joseph Mziku na kulia ni Steven Minja

Mkuu wa Kitengo cha Uthibi Ubora Chuo cha Bahari Fortunata M Kakwaya akimkaribisha Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na Tafiti kwa ufunguzi wa mafunzo

Mtaalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania Steven Minja akitoa mafunzo kwa Maofisa wa chuo cha bahari DMI.

Maofisa mbalimbali wakifuatilia kwa umakini mafunzo.

Mtaalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania Joseph Mziku akiendelea kutoa mafunzo.

Maofisa mbalimbali wakifuatilia kwa umakini mafunzo.

Maofisa mbalimbali wakifuatilia kwa umakini mafunzo.

Mtaalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania Steven Minja akitoa mafunzo kwa Maofisa wa chuo cha bahari DMI.