NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI MHE.ATUPELE AWATAKA WAKUU WA TAASISI WALIO CHINI YA WIZARA KUTENGA BAJETI YA MICHEZO KWA WATUMISHI..

21 Jan, 2023
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI MHE.ATUPELE AWATAKA  WAKUU WA TAASISI WALIO CHINI YA WIZARA KUTENGA BAJETI YA MICHEZO KWA WATUMISHI..

Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Atupele Mwakibete awataka wakuu wa Taasisi  walio chini ya Wizara kutenga bajeti ya Michezo ili kuwawezesha watumishi wao kushiriki kikamilifu kwenye michezo mbalimbali inayoandaliwa na Serikali ikiwemo SHIMIWI.

Naibu ameyazungumza hayo leo alipokuwa kwenye ufunguzi wa Bonanza la Watumishi wote waliopo chini ya Wizara ya Ujenzi lililofanyika kwenye viwanja vya michezo vya chuo kikuuu cha Dar Es Salaam.

"Niwatake Taasisi zote ambazo hazikushiriki michezo ya  SHIMIWI ijipange kushiriki na bajeti itengwe ili kuwawezesha watumishi kushiriki kikamilifu kwani ndio sehemu pekee inayowaunganisha kwa pamoja na kuleta umoja na mshikamano baina ya watumishi wote"  Alisema.

Aidha katika bonanza hili Chuo cha DMI kilifanikiwa kuondoka na medali mbili zikiwakilisha ushindi wa pili wa mbio za mita 100 kwa kuweka yai mdomoni na mbio za magunia za mita 100.

Bonanza la leo lililolenga kuwakutanisha watumishi wote wa Wizara kwa pamoja na kujenga mahusiano baina yao limejumuisha michezo ya mpira wa miguu, kukimbia kwa magunia, kutembea na yai likiwa mdomoni na kuvuta kamba.

 

Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Atupele Mwakibete akisikiliza ahadi ya Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari (DMI), Dkt.Tumaini Gurumo,  ya mchango wake kwa Mtumishi wa Wizara aliyeandaa Jarida la Klabu ya Uchukuzi zawadi iliyotolewa kama motisha kwake.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari (DMI), Dkt.Tumaini Gurumo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ziloizoshiriki bonanza hilo la michezo.

 

Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Atupele Mwakibete akitoa maelekezo kwa Viongozi Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuandaa  bajeti ya michezo ili kuwezesha watumishi kushiriki michezo mbalimbali inayoandaliwa na Serikali.

Picha ya Pamoja  Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari (DMI), Dkt.Tumaini Gurumo pamoja na wachezaji wa mpira wanaowakilisha DMI

Kaimu Mkuu wa Chuo cha DMI, Dkt. Tumaini Gurumo akisalimiana  na viongozi wa mpira wa miguu ya watumishi wa DMI kabla ya kuanza mashindano

 

 

Picha ya Pamoja ya Kaimu Mkuu wa Chuo cha DMI Dkt. Tumaini Gurumo na watumishi  kabla ya mashindano ya bonanza kuanza.

 

Watumishi wa DMI wakijiandaa na mchezo wa Mpira.

Watumishi wa DMI wakicheza mpira wa miguu na Taasisi ya TASAC

 

 

Watumishi wa DMI wakijiandaa kucheza mchezo wa Kuvuta kamba.