NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI MHE. DAVID M. KIHENZILE ATEMBELEA CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM

23 Nov, 2023
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI MHE. DAVID M. KIHENZILE ATEMBELEA CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM

Na Kitengo cha Masoko na Mawasiliano

Mhe. David M. Kihenzile (MB), Naibu Waziri wa Uchukuzi jana amefanya ziara katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam yenye lengo la kujitambulisha na kujionea shughuli zinazofanywa na chuo cha Bahari Dar es Salaam.

Akiwa chuoni hapo, Mhe. Kihenzile alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya chuo ikiwa ni pamoja na Kituo cha kufundishia lugha ya kiingereza kwa mabaharia, karakana  na kujionea mitambo mbalimbali ya kufundishia.

Mhe. Kihenzile ameipongeza menejimenti ya chuo cha Bahari Dar es Salaam kwa jitihada za kutaka kukipanua chuo hicho kwa kufikiria kuanziasha Kampasi mkoani Lindi kwa lengo la kendana na ongezeko la wanafunzi.

Alisema, Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani, Rias wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imewezekeza fedha Tirioni moja katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji kwa lengo la kukuza uchumi utokanao na sekta hiyo, “Maono yenu yamefika wakati muafaka, hivyo serikali inaahidi kuwaunga mkono katika maono yenu” Mhe. Kihenzile alisisitiza

Ameiagiza Menejimenti ya chuo cha DMI kuandaa taarifa inayoelezea ndoto ya chuo ya kutaka kujenga chuo kikubwa cha masuala ya Bahari kuendana na kasi ya ongezeko la wanafunzi.

Pia Mhe. Kihenzile ameisisitiza menejimenti kuendelea kutoa elimu bora itakayotengeneza vijana bora wenye uwezo kwani kwa kufanya hivyo nchi ya Tanzania itaendelea kuheshimiwa ndani na nje ya nchi na kutapunguza ajali nyingi za majini

Ameikumbusha Menejimenti ya DMI kuwa na wajibu kwa Taifa kwa kusimamia na kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakuwa na ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha zitakazotolewa na kwa kufanya hivyo wataepukana na hoja za ukaguzi.

Mwisho, Mhe. Kihenzile ameagiza chuo kiwe na mfumo wa kushughulikia maagizo ya viongozi wa serikali kwa kuteua mtu maalum wa kufuatilia maagizo na namna ya kuyasghulikia.