RADA YA KISASA IMEFUNGWA KATIKA CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM KWA AJILI YA KUJIFUNZIA

24 Sep, 2022
RADA YA KISASA IMEFUNGWA KATIKA CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM KWA AJILI YA KUJIFUNZIA

Rada ya kisasa imefungwa katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam ijulikanayo kwa jina la Live Radar yenye uwezo wa kuchukua na kuonyesha matukio halisi moja kwa moja baharini.

Rada hiyo ina uwezo wa kuona masafa marefu imenunuliwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Elimu ya Mafunzo ya Bahari (METFUND) kwa gharama ya fedha za kitanzania shilingi Milioni Mia mbili na ishirini na moja (Tsh. 221,000,000) iliyotengenezwa na Kampuni ya FURUMO kutoka Japan imefungwa kwa lengo la kufundishia.

Rada hiyo itatumika melini na kwenye minara ya kuongozea meli kuingia bandarini ina mfumo wa kuchakata taarifa za picha ili kupata uelekeo, kasi na umbali ambavyo husaidia kuepusha meli kugongana.

Aidha Rada hii ni ya kipekee ambayo hupatikana kwenye meli za kisasa ambazo nyingi hazipo nchini hivyo itasaidia zaidi wanafunzi kujifunza kwa vitendo kwa kutumia Rada hiyo