ELIMU NA UJUZI UTUMIKE KULETA UFANISI KATIKA SHUGHULI ZA BAHARI - NW KIHENZILE

07 Dec, 2024
ELIMU NA UJUZI UTUMIKE KULETA UFANISI KATIKA SHUGHULI ZA BAHARI - NW KIHENZILE

aibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Mwakiposa Kihenzile (Mb) amewapongeza wahitimu wa chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) na kuwataka kutumia vyema ujuzi waliopata katika kuleta ufanisi katika shughuli za Bahari ili kukuza Uchumi wa nchi.

Mhe. Kihenzile ametoa wito huo leo tarehe 06/12/2024 alipokuwa akiwatunuku wahitimu wa mwaka wa masomo 2023/2024 katika hafla  ya mahafi ya 20 ya DMI yaliyofanyika kwenye viwanja vya karimjee Jijini Dar es Salaam.

 Mhe Kihenzile amewasisitiza wahitimu kuhakikisha kwamba jitihada zilizofanywa na Serikali katika kuendeleza shughuli za Chuo zinathibitika na kuzaa matunda kupitia kazi zao ikiwa ni Pamoja na, kujiendeleza, kuwa wabunifu na kutafuta ujuzi zaidi katika sekta ya Bahari kwani sekta inakuwa kila siku kulingana na mabadiliko.

Kati ya wanafunzi 1506 waliohitimu leo, Wanawake ni 433 na Wanaume 1073 ambapo miongoni mwao wako wanafunzi 72 wa Shahada ya Uzamili, 344 wa Shahada, 242 wa Stashahada, 401 wa Astashahada, 417 wa Astashahada ya Awali pamoja na wanafunzi wapatao 30 wa vyeti vya umahiri (CoC) Maafisa wa Melini Daraja la tatu, na la pili.