DMI YAWASHUKURU WADAU WA ELIMU YA JUU KWA MICHANGO YA UHUISHAJI MITAALA

18 Oct, 2023
DMI YAWASHUKURU WADAU WA ELIMU YA JUU KWA MICHANGO YA UHUISHAJI MITAALA

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt. Wilfred J. Kileo amewashukuru Wadau wa balimbali kwa michango yao waliyoitoa yenye lengo la kuboresha mitaala iliyotengenezwa na inayohuishwa ili iendane na uhalisia wa soko kabla ya kupelekwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa ajili ya ithibati na matumizi.

Akizungumza wakati wa kufunga majadiliano hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Bahari leo amesema kuwa, mitaala hii iliyohuishwa inalenga kuzalisha wataalamu ambao wataendana na mahitaji ya soko na wakati kulingana na taaluma watakazosomea.

“Tunawashukuru kwa muda wenu na michango mliyotoa, tunaheshimu sana michango yenu na tunaahidi kufanyia kazi , hii ni hatma ya vijana wetu, Hivyo ni vyema kuhakikisha kwamba tunamuandaa kijana ambaye ataendana na uhalisia kulingana na kile alichosomea”Alisema Dkt.Kileo

Warsha ya majadiliano ya uhuishwaji mitaala ya Chuo cha Bahari Dares salaam ilianzia kwenye upembuzi na sasa imefikia hatua ya ukamilishaji.