DMI YAWAFIKIA WAKAZI WA TANGA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU

26 May, 2024
DMI YAWAFIKIA WAKAZI WA TANGA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU

Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) kinashiriki maadhimisho ya wiki ya Elimu, Ujuzi na Ufundi yanayofanyika Tanga kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari  Popatlal kuanzia tarehe 25-31 Mei, 2024.

Wataalamu wa Chuo Cha Bahari Dar es Salaam wapo kutoa huduma kuhusu Elimu na Mafunzo yanayotolewa DMI, kutoa ushauri kwa Wazazi na Wanafunzi kuhusu sifa za kujiunga na Chuo pamoja na Ushauri wa Kozi za kusoma kulingana na ufaulu wa mwanafunzi.

Tunakaribisha Wazazi, Walezi na Wanafunzi waliopo Tanga na maeneo ya jirani kutembelea Banda la Chuo Cha Bahari Dar es Salaam ili kupata uelewa wa fursa zilizopo kwenye Sekta ya Bahari na Maji kwa Ujumla.

DMI-Kituo Cha Ubora Cha Elimu na Mafunzo ya Bahari.