DMI YATAKIWA KUHAMASISHA VIJANA WA KIKE KUJIUNGA NA FANI ZA UBAHARIA

25 Sep, 2023
DMI YATAKIWA KUHAMASISHA VIJANA WA KIKE KUJIUNGA NA FANI ZA UBAHARIA

Waziri wa Uchukuzi Mhe.Prof.Makame M. Mbarawa amekitaka Chuo cha Bahari Dar es Salaam kuongeza jitihada za kuhamasisha Vijana wa kike kujiunga na fani za ubaharia ili kuongeza idadi ya wataalamu wa kike kwenye sekta usafirishaji kwa njia ya maji kama ilivyo kwenye sekta ya anga..

Waziri ameyazungumza hayo leo alipokuwa akifungua maonesho ya wiki ya maadhimisho ya siku ya Bahari duniani, yanayofanyika Kitaifa Zanzibar-Pemba kwenye viwanja vya Gombani kuanzia tarehe 25 hadi 28  Septemba 2023.

Mhe Makame amesema kuwa kumekua na muitikio mdogo sana kwa watoto wa kike kujiunga na fani za masomo ya Ubaharia wakati ni fani zinazosomwa na vijana wa jinsi zote yaani wakike na kiume.

“Fani hizi za Ubahari sidhani kama ni ngumu kama vijana wengi ambavyo hudhani na kuona kama ni fani za kiume pekee, Ubaharia ni taaluma nzuri, ni wakati sasa kuona namna bora ya kufanya ili kuhamasisha vijana wa kike kujiunga na fani za ubaharia ili kuwainua kiuchumi lakini pia kwa maendeleo ya Taifa kwa Ujumla”Alisema Mhe.Makame

Ameongeza kuwa , asilimia kubwa ya Uchumi wa Dunia unategemea usafiri wa maji, ni muhimu kuwa na vijana wa jinsi zote  kwenye sekta hii  kama  ilivyo kwenye anga ili kupanua wigo wa fursa za ajira ndani na nje ya Nchi.

Tanzania kupitia Sekta zote za Usafiri kwa njia ya maji zinaungana na Dunia kuadhimisha  kilele cha siku ya bahari ambayo hufanyika kila Alhamisi ya mwisho wa mwezi wa tisa, Pemba siku hizo zitatumika kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutunza mazingira ya bahari, kuelimisha wanafunzi fursa zitokanazo na masomo ya fani za ubaharia katika kushagisha Sera ya Uchumi wa Buluu na kutoa msaada (CSR) kwa vivuko vilivyopo pemba.

Maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani kwa mwaka 2023 yamebebwa na kauli mbiu ya “MIAKA 50  YA MARPOL: UWAJIBIKAJI WETU UNAENDELEA”.

 

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo akitoa salamu za Chuo wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya maonesho ya siku ya Bahari yanayofanyika kwenye viwanja vya Gombani, Pemba.

Katika picha ya pamoja ni Mwenyekiti wa Bodi ya DMI Kapteni. Ernest Bupamba wa tatu kushoto, Mkuu wa Chuo cha bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo wa pili kushoto, Kaptain Haruna Ally Mhadhili wa Chuo cha Bahari DMI wa kwanza kushoto na Injinia Daniel Lukono Mhadhili wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam.

Injinia Daniel Lukono na Mhadhili wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam akitoa elimu kwa wageni waliotembelea Banda la Chuo Cha Bahari kwenye maonesho ya maadhimisho ya  Wiki ya Bahari Duniani

Kaptain Haruna Ally na Mhadhili wa Chuo cha Bahahari Dar es Salaam akitoa ufafanuzi wa elimu inayotolewa chuoni kwa mgeni aliyetembelea banda  la Chuo cha Bahari kwenye maoneshoya maadhimisho  ya wiki ya siku ya Bahari Duniani yanayofanyika Pemba -Gombani.

 

Injinia Daniel Lukono na Mhadhili wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam akitoa elimu kwa mwanafunzi alipotembelea Banda la Chuo Cha Bahari kwenye maonesho ya maadhimisho ya  Wiki ya Bahari Duniani

Kaptain Haruna Ally na Mhadhili wa Chuo cha Bahahari Dar es Salaam akitoa ufafanuzi wa elimu inayotolewa chuoni kwa mgeni aliyetembelea banda  la Chuo cha Bahari kwenye maoneshoya maadhimisho  ya wiki ya siku ya Bahari Duniani yanayofanyika Pemba -Gombani.

Injinia Daniel Lukono na Mhadhili wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam akitoa elimu kwa mgeni alipotembelea Banda la Chuo Cha Bahari kwenye maonesho ya maadhimisho ya  Wiki ya Bahari Duniani