DMI YAPONGEZWA KWA KUWA MSINGI BORA WA TAALUMA YA BAHARI
05 Dec, 2024
Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) kimepongezwa kwa kazi kubwa ya kuzalisha rasilimali wenye weredi na kuwa msingi bora wa taaluma za sekta ya usafiri kwa njia ya maji kupitia elimu na mafunzo inayotolewa .
Pongezi hizo zimetolewa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa shirika la bandari Zanzibar (ZPC) Bw. Joseph Abdallah Meza alipokuwa akifungua kongamano la tatu la kitaalamu (Convocation) lililofanyika kwenye ukumbi wa DMItarehe 04/12/2024