DMI YAINGIA MKATABA WA KUBADILISHANA UZOEFU NA CHUO CHA ITALY.

Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimeingia makubaliano ya Mashirikiano ( MoU) na Chuo cha Italian Shipping Academy Kilichopo nchini Italy.
Makubaliano haya yamefanyika Nchini Italy kati ya Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo tarehe 19/10/2023 kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika mafunzo ya ubaharia na kushirikiana katika tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha DMI Dkt. Tumaini Gurumo amesema kuwa makubalino hayo ya Miaka mitano yatasaidia kuongeza ujuzi kati ya Wanafunzi na Wahadhiri kwa pande zote mbili.
“Nimefurahi sana kuingia Makubaliano haya kwakua wenzetu wapo tayari kushiriana nasi katika miradi mbalimbali, ninaona ndoto ya kufikia viwango vinavyokubalika na EU inakwenda kutimia” Alisema Dkt. Tumaini.
Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Mbalozi kutoka Tanzania Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Italy nchini Tanzania Balozi Marco Lombardi.
Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema kuwa wenzetu wapo mbele kiteknolojia na Mafunzo na wapo tayari kufanya kazi na DMI, hivyo ni muhimu nasi tuwe tayari na kufanya jitihada kuonyesha ushirikiano ili uhusiano uzae matunda.
Naye Mkuu wa Chuo cha Italian Shipping Academy Foundation (FAIMM) Eugenio Massolo amesema kuwa makubaliano hayo yatasidia kukuza ujuzi kwa pande zote mbili ili kuendana na uhitaji wa soko la Ajira.
Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo wakipeana mkono wa shukurani baada ya kusaini nyaraka za makubaliano.
Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo yakishuhudiwa na Balozi wa Tanzania Nchini Italy Balozi Mahmoud Thabit Kombo
Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo