DMI,TASAC NA MAMLAKA YA BAHARI YA BAHAMAS LONDONI UINGEREZA KUSHIRIKIANA KUKUZA SEKTA YA USAFIRI MAJINI.

06 Jun, 2023
DMI,TASAC NA MAMLAKA YA BAHARI YA BAHAMAS LONDONI UINGEREZA KUSHIRIKIANA KUKUZA SEKTA YA USAFIRI MAJINI.

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Dkt. Tumaini Shabani Gurumo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Kaimu A. Mkeyenge na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Ajira za Mabaharia, Capt. Oli Olsen wakutana katika Ofisi za Mamlaka ya Bahari ya BAHAMAS mjini London, Uingereza tarehe 05 Juni, 2023 kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya sekta ya usafiri majini.

Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na kutambuliana vyeti vya mabaharia (Recognition of Seafarers Certificate) na mafunzo kati ya DMI, TASAC na Mamlaka ya Bahari ya BAHAMAS.

Halikadhalika, walizungumzia pia suala la Mabaharia wa kitanzania kupatiwa mafunzo katika meli zilizosajiliwa na Mamlaka ya Bahari ya BAHAMAS.

Kwa upande wake Capt. Oli kwa niaba ya Mamlaka ya Bahari ya BAHAMAS ameahidi kushirikiana na Mamlaka zinazosimamia masuala ya Mabaharia nchini yaani DMI na TASAC Tanzania hususan katika maeneo ya kutambualiana vyeti na mafunzo ili kukuza sekta ya usafiri majini nchini Tanzania.

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Dkt. Tumaini Shabani Gurumo (Wa kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Kaimu A. Mkeyenge (Wa katikati) na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Ajira za Mabaharia, Capt. Oli Olsen (Wa kwanza Kulia) walipokutana katika Ofisi za Mamlaka ya Bahari ya BAHAMAS Mjini London.

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Dkt. Tumaini Shabani Gurumo (Wa kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Ajira za Mabaharia, Capt. Oli Olsen (Wa kwanza Kulia) walipokutana katika Ofisi za Mamlaka ya Bahari ya BAHAMAS Mjini London.