DMI YAIMARISHA UWEZO WA WATUMISHI KATIKA USIMAMIZI WA MAAFA
Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), leo tarehe 28 Oktoba 2026, kimeendesha mafunzo ya Usimamizi wa Maafa (Disaster Management) kwa watumishi wake katika Ukumbi wa Chuo.
Mafunzo hayo yametolewa na wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Usimamizi wa Maafa, kwa lengo la kuimarisha uelewa na uwezo wa watumishi katika kujiandaa na kukabiliana na maafa.
Akifungua mafunzo hayo, Makamu Mkuu wa Chuo wa Taaluma, Prof. Wilfred Kileo, aliwasihi watumishi kuzingatia na kutumia ipasavyo maarifa watakayoyapata. Alisisitiza kuwa usimamizi wa maafa ni muhimu katika kuimarisha usalama na ni sehemu ya wajibu wa kitaasisi na kitaifa.
Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za DMI za kuimarisha utayari wa Taasisi katika kuzuia na kupunguza athari za maafa, kujiandaa na kukabiliana nayo, pamoja na kulinda maisha na mali. Hatua hiyo inalenga kuchangia katika kujenga mazingira salama kwa watumishi na wanafunzi, huku ikiimarisha uwezo wa Taasisi kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa maafa.
