DMI YAPOKEA UJUMBE KUTOKA SERIKALI YA SHIRIKISHO LA SOMALIA

Published: Aug 27, 2026
DMI YAPOKEA UJUMBE KUTOKA SERIKALI YA SHIRIKISHO LA SOMALIA cover image



Chuo cha Baharia Dar es Salaam (DMI) tarehe 16 Julai 2026 kilipokea ujumbe kutoka Serikali ya Shirikisho la Somalia uliotembelea Chuo kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu elimu na mafunzo ya sekta ya usafiri kwa njia ya maji pamoja na shughuli mbalimbali za Uchumi wa Buluu zinazotekelezwa na Chuo.

Akipokea ugeni huo, Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Fedha, Mipango na Utawala, Prof. Lucas Mwisila, aliushukuru ujumbe huo kwa kuchagua DMI kama sehemu ya kujifunza na kubadilishana uzoefu. Aidha, aliwakaribisha kuendelea kutembelea Chuo wakati wowote ili kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Kwa upande wake, kiongozi wa ujumbe kutoka Serikali ya Shirikisho la Somalia, Bw. Ahmed Warsame, aliipongeza DMI kwa kazi nzuri inayofanya na kueleza kuwa ameridhishwa na mambo yote waliyojifunza. Alisema watafanyia kazi uzoefu walioupata na kuialika DMI kutembelea Mogadishu kwa ajili ya kuendelea kubadilishana uzoefu.