WAFANYAKAZI WA DMI WAUNGANA KUSHEREHEKEA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

01 May, 2023
WAFANYAKAZI WA DMI WAUNGANA  KUSHEREHEKEA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

Watumishi wa Chuo cha Bahari Dar es salaam wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Fedha na Mipango Dkt. Wilfred Kileo wameungana na watanzania wote Nchini kusherehekea siku ya wafanyakazi Duniani.

Sherehe hizo hufanyika kila tarehe 1 ya mwezi Mei ambapo kwa mwaka huu 2023, wafanyakazi wamekutana katika viwanja vya Uhuru Jijini Dar es Salaam huku kitaifa ikiadhimishwa Mkoani Morogoro.

Maadhimishon ya wafanyakazi mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu ya "Mishahara Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa maendeleo ya Wafanyakazi,Wakati ni sasa"

Makamu Mkuu wa Chuo Fedha na Mipango Dkt. Wilfred Kileo, akiwa kwenye meza kuu katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yaliadhimishwa kwenye viwanja vya Uhuru Jijini Dar es Salaam

Wafanyakazi wa Chuo cha Bahari (DMI) wakiwa kwenye matukio mbalimbali , ikiwa ni sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani.