WATUMISHI DMI WATAKIWA KUDUMISHA USHIRIKIANO MAHALA PA KAZI

17 Feb, 2023
WATUMISHI DMI WATAKIWA KUDUMISHA USHIRIKIANO MAHALA PA KAZI

Watumishi wa Chuo cha Bahari Dar Es Salaam watakiwa kudumisha ushirikiano katika utendaji kazi ili kuyafikia matarajio yaliyowekwa na Chuo ikiwa ni pamoja na yale yaliyowekwa Kitaifa yanayopaswa kutekelezwa na Chuo.

Hayo yamezungumzwa leo na Kaimu Mkuu wa chuo cha Bahari (DMI) na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi , Dkt.Tumaini Gurumo alipokuwa kwenye kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo kwa lengo la kupitia makisio ya mapato na matumizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo jumla ya Bilioni 21.47 imeridhiwa na kupitishwa.

Akirejea katika mjadala wa mafanikio ambayo chuo imekipata katika muendelezo wa bajeti inayotarajiwa kuisha Juni 2023, Mkuu wa chuo amesema , mafanikio yote yanayoonekana yametokana na umoja na ushirikiano uliopo baina ya watumishi na kila mtu akifanya kazi katika nafasi yake kwa weredi mafanikio ya chuo hayana budi kuonekana.

Aidha ameshukuru uongozi wa chama cha wafanyakazi cha RAAWU ngazi ya Kanda kufika chuoni kushiriki kikao hicho.

Katibu wa Chama cha wafanyakazi cha RAAWU Kanda, Bi.Eva Mrosso ameishukuru menejimenti ya chuo kwa maandalizi ya kikao na ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa kwa chama na kwamba wanayaona mabadiliko na wao kama chama wapo tayari kutoa ushirikiano wowote ambao chuo utahitaji.

Mbali na kujadili makisio ya mapato na matumizi ya Bajeti, Baraza pia limeweza kujadili namna bora ya kupanua wigo wa kuongeza mapato ya ndani  pamoja na mafanikio na mipango ya mbeleni katika kuhakikisha utoaji wa huduma ya Elimu na Mafunzo unakuwa wa kiwango cha Kimataifa kama ambavyo  Chuo kinavyotambulika kwa ukubwa wake.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari (DMI) na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi , Dkt.Tumaini Gurumo akisistiza umoja na ushirikiano baina ya wanafunzi kwa mustakabali wa maendeleo ya Chuo na Taifa kwa ujumla.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari (DMI) na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi , Dkt.Tumaini Gurumo akichangia mada mara baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo ya mapato na matumizi.

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha DMI.

Mkuu wa Idara ya Mipango Ndg.Anderson Tweve (wa kwanza kulia) akiwasilisha mapendekezo ya mapato na matumizi ya Bajeti ya Mwaka 2023/2024 kwa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi leo kwenye ukumbi wa Chuo.

Mkuu wa Idara ya Mipango Ndg.Anderson Tweve akichukua maoni ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi  mara baada ya kuwasilisha mapendekezo ya Bajeti.

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha DMI.

Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha DMI.

Katibu wa Chama cha wafanyakazi cha RAAWU Kanda, Bi.Eva Mrosso (katikati) akichangia mada wakati wa uwasilishwaji wa bajeti na kushukuru Menejimenti ya chuo kwa ushirikiano wao katika Chama cha wafanyakazi RAAWU.