NAIBU KATIBU MKUU DKT. POSSY AWATAKA DMI KUJITANGAZA

22 Feb, 2022
NAIBU KATIBU MKUU DKT. POSSY AWATAKA DMI KUJITANGAZA

Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Dkt. Ally Possi, akisisitiza jambo kwa Uongozi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa kitengo cha Usafishaji Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Kapteni Haruna Ally, akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Dkt. Ally Possi, kuhusu mashine za kuendeshea meli zinavyotumika, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Dkt. Ally Possi, akimsikiliza Mhandisi Daisim Mlay kuhusu utendaji kazi wa mashine zilizopo ndani ya meli, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Victor Kilindo kutoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) akiemweleza Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi matumizi mbalimbali vifaa vya ukoaji wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Kapteni Haruna Ally kutoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) Haruna Ally akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi kuhusu namna meli inavyoshushwa kutoka kwenye meli, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Dkt. Ally Possi, akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI, Prof. Erick Massami baada ya kukagua eneo la chuo hicho lilipo bandarini, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea chuo hicho jijini Dar es Salaam.