NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA ATEMBELEA CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM (DMI)

12 Oct, 2022
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA ATEMBELEA CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM (DMI)

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Juma Kipanga (MB) amefanya ziara ya kutembelea katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) na kujionea shughuli mbalimbali zinazohusiana na tasnia ya bahari

Katika ziara hiyo aliyoifanya tarehe 10/10/2022, Mhe. Omary Juma Kipanga ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mafia lakini pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, amesema kuwa lengo la ziara yake katika chuo hicho ni kutaka kujifunza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na fursa zilizopo baharini ili aweze kuitumia elimu atakayoipata katika kuwanufaisha wananchi wa Jimbo lake la Mafia, “Nimekuja kujifunza kutoka kwenu”, Alisema

Kutokana na Jimbo hilo kuzungukwa na bahari, wananchi wa eneo hilo shughuli zao kuu za kiuchumi, biashara na kijamii wanategemea sana uwepo wa bahari ya hindi, hivyo ameona ni vyema atembelee chuo cha bahari Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza Zaidi. 
Mhe. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya chuo ikiwa ni pamoja na karakana ambapo wanafunzi wanasoma kwa vitendo, aidha amefurahi kujifunza mengi yahusuyo bahari kwa maslahi ya wananchi wa Jimbo la Mafia.

Dkt. Werneld Ngongi  akielezea namna umeme unavyofanya kazi melini 

Mhandisi Miraji mkwambe (Kulia) akitolea ufafanuzi wa matumizi ya mashine mbalimbali

 Naibu Waziri akiwa katika Chumba cha mitambo (Simulation Room) akijifunza jambo kutoka kwa Mhandisi Isack Lazaro 

Capt. Hilary salumu (Kushoto) akipokea maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri

Capt. Hilary salumu (Kushoto) akipokea maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri