CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM KATIKA VIWANJA VYA MAONESHO YA NANENANE– MBEYA

05 Aug, 2022
CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM KATIKA VIWANJA  VYA MAONESHO YA NANENANE– MBEYA

Chuo cha Bahari Dar Es Salaam katika viwanja vya Nanenane vya John Mwakangale vilivyopo Jijini Mbeya kimeendelea na harakati za kuelezea fursa mbalimbali zitolewazo na chuo hicho katika kukuza uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja kufuatana na kauli mbiu ‘Kilimo ni biashara shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo, Mifugo na Uvuvi’.

Katika kutekeleza Kauli mbiu ya Maonesho ya Nanenane 2022 isemayo, “Kilimo ni Biashara,Shiriki  kuhesabia kwa mipango bora ya kilimo, Mifugo na Uvuvi”, Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) ndicho chuo pekee chenye ithibati ya kimataifan  chini Tanzania, Afrik Mashariki na Kati kinachoandaa wataalam katika sekta ya bahari wakiwemoWahandisi waMeli, Manahodha na mabaharia wengine wanaojihusisha na usafirishaji wa mazao na malighafi zote kwa kutumia meli katika hali ya usalama.

Mhandisi Deism D Mlay alisema, Kutokana na wataalam wanaohitimu katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam, kunawezesha kuwa na usafiri wa uhakika nchini ambapo wawekezaji watavutiwa kuja kuwekeza kwakuwa watakuwa na uhakika wa kusafirisha mazao na malighafi nyingine zitokanazo na kilimo kutoka sehemu moja kwenda nyingine,hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.

Wageni mbalimbali katika banda la Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) 

Dkt. Wilfred J. Kileo akiwaelezea jambo wageni waliotembelea katika banda la DMI              

Bi .Rehema Juma (Msajili) akielezea fursa za masomo zitolewazo na chuo cha DMI 

Mhandisi DeismD. Mlay akielezea namna ya kujiokoa majini wakati wa dharula kwa kutumia kifaa maalum kiitwacho ‘Life Raft’

Mhandisi Deism D.Mlay akiwaonesha wageni video ya namna ya kujiokoa kwa kutumia kifaa maalum  kitwacho ‘Life Raft’ 

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Usajili kutoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) Ndugu Bernad Mgendwa akielezea fursa zitokanazo na tasnia ya bahari 

Wanafunzi wapatao 762 kutoka sekondari mbalimbali katika Halmashauri 7 za Mkoa wa Mbeya wakiwa katika kambi ya UMISETA iliyopo katika sekondari ya Iyunga mkoani Mbeya walipata fursa ya kutembelewa na wataalam kutoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam