CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM (DMI) KUTOA MAFUNZO YA MANUFAA YA UCHUMI WA BULUU KWA VIJANA.

Mkuu wa chuo cha Bahari Dar es Salaam Prof. Tumaini Gurumo amesema kuwa chuo cha bahari Dar es Salaam (DMI) kimeona fursa nyingi katika uchumi wa buluu hivyo kinatazamiwa kuanzisha mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa vijan kusiana na manufaa katika uchumi wa buluu.
Prof. Gurumo ameyasema hayo kwenye kongamano la uchumi wa buluu lililofanyika jiji Banjul nchini Gambia.
“Kweli katika kongamano hili tumekubaliana nchi zote za Afrika kutumia vyanzo vyetu vya maji kama vila bahari, mito mabwawa, maziwa na vyanzo vingine kuhakiisha vinasaidia jamii za kiafrika kiuchumi, hivyo sisi DMI tutaendelea kutoa Elimu na mafunzo kwa vijana kuonyesha fursa za Uchumi wa Buluu” Asema Gurumo
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Uchukuzi Bi Stella Katondo amesema kuwa kongamo hilo ni muhimu sana kwa maendeleo na manufaa ya uchumi wa buluu. Hivyo kwa chuo cha DMI kimepata nguvu ya kuendelea kutoa elimu ya umuhimu wa uchumi wa buluu.
Naye mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka shirika la uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bi. Leticia Mutaki amesema kuwa kupitia kongamano hilo TASAC itaendelea na kazi ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira katika vyanzo vya maji ili viumbe walipo waendele kuishi kwa manufaa ya mazingira na wananchi.
Katika Kongamano lilifanyika kwa siku tatu likiwakutanisha wataalamu kutoka nchi zaidi ya kumi na sita ambao walikubaliana kushirikiana kuweka nguvu ya pamoja kuhakikisha vyanzo vya maji vilivyopo Afrika vina wanufaisha wanchi wote wa Afrika.