CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM (DMI) CHASHIRIKI SIKU YA MABAHARIA DUNIANI

23 Jun, 2024
CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM (DMI) CHASHIRIKI SIKU YA MABAHARIA DUNIANI

Chuo cha Bahari Dar Es Salaam (DMI) kimeshiriki katika maonesho ya Siku ya Mabaharia Duniani ambayo kitaifa yanaadhimishwa katika viwanja vya Nia Njema vilivyopo katika vilaya ya Bagamoyo – Mkoa wa Pwani.

Maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Uchukuzi yamehusisha taasisi mbalimbali za serikali na wadau wa tasnia ya Bahari yameanza leo tarehe 22 – 25/06/2024 yamefunguliwa na Mhe. Dkt. Khalid Salumu Mohamed, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Lengo la maadhimisho ya siku ya mabaharia ni kutambua mchango unaotolewa na mabaharia duniani na kitaifa hususan katika Nyanja za kibiashara, Uchumi na jamii kwa ujumla.

Maadhimisho hayo yataambatana na kufanya usafi katika baadhi ya fukwe za Bahari na kutembelea baadhi ya mialo kwa lengo la kutoa elimu kwa wavuvi wadogo wadogo kuhusiana na usalama majini.