WATUMISHI WA DMI WAPATIWA MAFUNZO YA HUDUMA KWA MTEJA

16 Mar, 2022
WATUMISHI WA DMI WAPATIWA MAFUNZO YA HUDUMA KWA MTEJA

Watumishi wa DMI wapatiwa mafunzo ya Huduma kwa Mteja

Idara ya Raslimali Watu imeratibu na kuendesha mafunzo ya huduma kwa mteja kwa watumishi wa chuo cha Bahari Dar es Salaam tarehe 02/03/2022.

Akiwa anafungua mafunzo hayo, Mkuu wa chuo cha Bahari Dar es Salaam, Prof. Erick P. Massami, aliwahimiza watumishi kushiriki kikamilifu na kupokea mafunzo kwa manufaa ya Chuo cha Bahari

Mkuu wa Idara ya Raslimali Watu, Ms. Monica Ngowo aliwataka watumishi kuwa wasikivu kwa kuwa mafunzo hayo ni ya msingi katika kuwahudumia wateja wa ndani na nje

Mwezeshaji Dkt. Charles Rweiyakaza aliwasisitiza washiriki kuwa waadilifu kwa wateja katika kutoa huduma kwa kuzingatia viwango na weledi ili kuepuka malalamiko

Washiriki wa mafunzo ya huduma kwa mteja wakisikiliza kwa makini