DMI YATOA VYETI KWA WAHITIMU TISA (9) WALIODHAMINIWA NA FAO

10 Jul, 2023
DMI YATOA VYETI  KWA WAHITIMU TISA (9) WALIODHAMINIWA NA FAO

Chuo cha Bahari Dar es Salaam leo kimetoa vyeti kwa wanafunzi 9 kutoka Tanzania, Kenya na Uganda waliodhaminiwa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi wao wanaofanyia kazi kwenye Idara za Uvuvi.

Akikabidhi vyeti hivyo kwenye ukumbi wa Chuo, Kaimu Mku wa Chuo Dkt. Lucas Mwisila (Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma) kwa niaba ya uongozi wa Chuo, aliwapongeza wanafunzi wote kwa jitihada walizozionyesha hatimae kufuzu masomo yao ambayo yaliendeshwa kwa kipindi cha wiki moja  kuanzia tarehe 3 hadi 10 Julai 2023. Ameongeza kuwa ujuzi wa mafunzo kwa vitendo waliyopata utawasaidia kaongeza umahiri na kujiamini katika majukumu yao.

Aidha washiriki hawa tisa kwa kipindi hiki cha wiki moja walifanikiwa kujifunza juu ya Personal Survival Techniques,Boat Operation Techniques, Navigation Skills, Fire Prevention and Fighting Skills,Medical First Aid at Wrking Training, Diving Technique, Boat Care and Maintainance Techniques, ICT and GIS Techniques ,Swimming and Life saving Skills.

Chuo kinatoa kozi  na programu mbalimbali za Bahari kwa watu binafsi  na Serikali  kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Komoro, Rwanda, Burundi, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Namibia. DMI inatambulika kwa programu zake za mafunzo ya ubora wa hali ya juu katika tasnia ya Bahari kwa kufuata viwango vya kimataifa.

Katika picha ni Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt.Lucas Mwisila (Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma) akikabidhi vyeti kwa wahitimu.

 

 

 

 

 

 

 

 

Picha ya pamoja baada ya hafla fupi ya utoaji vyeti.