Event: BARAZA LA WAHITIMU

BARAZA LA WAHITIMU

Siku ya Baraza la Wahitimu ni siku maalumu inayowakutanisha wahitimu, uongozi wa Chuo, watumishi na wadau mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea mafanikio ya kitaaluma, kutambua mchango wa wahitimu, kuimarisha uhusiano kati ya Chuo na wahitimu wake, pamoja na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Chuo, ikiwemo programu za elimu na mafunzo, huduma, maendeleo na mwelekeo wa Chuo kwa siku zijazo.