Taarifa za waliowahi kusoma Chuo cha Bahari (DMI) miaka ya nyuma

19 Nov, 2022

DMI Alumni Contact Information

Taasisi ya Bahari Dar es Salaam (DMI), inaanzisha kanzidata ya Wahitimu wake duniani kote ili kuboresha mawasiliano kati ya Taasisi na sekta ya Bahari kupitia kanzidata ya wanachuo. Taasisi inathamini umuhimu wa kuhifadhi data za wahitimu kwani inaleta mshikamano ambao una faida zifuatazo miongoni mwa nyinginezo: Kushiriki habari kuhusu fursa za ufadhili wa masomo na kushiriki katika mijadala ya kitaaluma, warsha za ushauri kuhusu elimu na masuala ya ajira. DMI inawaalika wahitimu wake wote kushiriki maelezo yao ya mawasiliano na kuahidi kwamba data iliyotolewa itawekwa siri na kutumiwa na DMI kwa ajili ya kufuatilia wahitimu na shughuli za wahitimu. Tafadhali jaza fomu fupi hapa chini na usaidie kusambaza fomu hii kwa wahitimu wenzako wa DMI

Bonyeza hapa kujisajili