WANAWAKE DMI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI, WAMEASWA KUDUMISHA UMOJA.

08 Mar, 2023
WANAWAKE DMI WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI, WAMEASWA KUDUMISHA UMOJA.

Wanawake wa Chuo cha Bahari Dar es salaam (DMI) waungana na wanawake wote duniani kusherehekea maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani ambayo hufanyika tarehe 8 machi,  kwa Mkoa wa Dar es salaam maadhimisho haya yamefanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja yakiongozwa na mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amosi Makalla.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amewapongeza wanawake wote kwa hamasa ya kushiriki maadhimisho hayo na kuwataka kudumisha umoja katika shughuli zao.

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki kuadhimisha siku hii  kwa sababu Nchi inatambua mchango wa mwanamke na kuthamini jitihada zake katika kuleta mafanikio na kuhamasisha  mabadiliko katika jamii .

Aidha ametoa wito kwa wanawake wajasiliamali kutengeneza bidhaa kwa kukidhi vigezo vya ubora ili bidhaa hizo ziweze kuuzika nje ya nchi na kuwaasa watanzania kujenga tabia ya kununua bidhaa zinazotengenezwa  na watanzania ili kukuza uchumi wetu.

Mkuu wa Mkoa amezitaka pia taasisi zinazosimamia bidhaa zinazotengenezwa na wajasiliamali kutowakatisha tamaa  wanawake na badala yake kuwatia moyo kwani wanawake wanaweza.

Maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani 2023 yamebeba kauli mbiu ya “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia, Chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia”.

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe.Amosi Makalla akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyoadhimishwa kimkoa kwenye viwanja vya mnazi mmoja leo.

 

Watumishi wanawake wa DMI wakiwa kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani  kwenye viwanja vya mnazi mmoja leo.

Watumishi wanawake wa DMI wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiongozwa na Mjumbe wa Bodi Dkt.Mwamini Tuli  (wa kwanza kulia ).

Watumishi wanawake wa DMI wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiongozwa na Mjumbe wa Bodi Dkt.Mwamini Tuli  (ameketi katikati).

Picha ya pamoja ya watumishi wa DMI

Picha ya pamoja ya watumishi wa DMI

Watumishi wanawake wa DMI wakiserebuka wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani  mnazi mmoja leo.

Watumishi wanawake wa DMI wakielekea kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani  kwenye viwanja vya mnazi mmoja leo.

Picha ya pamoja ya watumishi wanawake wa DMI mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mnazimmoja .

Picha ya pamoja ya watumishi wanawake wa DMI wakijiandaa kuelekea kwenye viwanja vya Mnazimmoja .

Watumishi wanawake wa DMI wakiwa kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani  kwenye viwanja vya mnazi mmoja leo.