WATUMISHI DMI WATAKIWA KUTUMIA BONANZA KUJIPANGA VIZURI KWA MAFANIKIO YA TAASISI NA TAIFA KWA MWAKA 2023
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar Es Salaam Dk.Tumaini Gurumo amesema kuwa mafanikio ya DMI mwaka 2022 yametokana na umoja wa utendaji kazi wa wafanyakazi hivyo, kuwataka kutumia siku ya bonanza la watumishi kujiweka tayari kimwili na kiakili kwa mafanikio yaliyo mbele yetu tunapoeleka mwaka 2023 kwa ustawi wa Taasisi na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa leo kwenye viwanja vya michezo vya Gwambina TTC vilivyopo Chang'ombe na Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na Tafiti Dk.Lucas Mwisila, alipokuwa akiwasilisha ujumbe wa kufunga bonanza uliotumwa kwa njia ya simu na kaimu Mkuu wa Chuo mbapo watumishi wote wa DMI walikutana kwenye bonanza la michezo lililolenga kujenga na kuimarisha mahusiano bora baina ya watumishi.
“Nawapongeza washiriki wote wa michezo kwa kushiriki kikamilifu bila kutegea, Kaimu Mkuu wa chuo ametuma ujumbe kwenu naomba niuwasilishe na liwe ndilo neno la kufungia bonanza letu” alisema Dkt.Mwisila.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi Bw.Mbaga Mshindi wa mbio za mita 200 na mfungaji bora wa magoli upande wa mpira wa miguu alisema anamshukuru Mkuu wa chuo, menejimenti na walimu wote walioandaa bonanza hilo lililo wakutanisha watumishi pamoja.
Gabriel Samason meneja wa timu ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi amepongeza DMI kwa kuandaa bonanza la michezo na kuwa mfano bora kwa Wizara, hivyo kuwataka kujiandaa vyema kwa michezo ya mpira wa miguu, mpira wa mikono na uvutaji kamba inayotarajiwa kufanyika tarehe 21 January ambapo taasisi 13 zilizopo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi zinatarajiwa kushiriki.
Bonanza la michezo DMI leo lilihusisha michezo ya mpira wa miguu,mikono na nyavu, kuvuta kamba, mbio za mita 100 na 200, kukimbia kwa magunia, bao,draft, rede na karata.
Mchezo wa riadha.
Mchezo wa kuvuta kamba
Mchezo wa mbio za magunia
Mchezo wa Karata
Mchezo wa Draft
Mchezo wa Bao
Mpira wa Pete au netibali
Mchezo wa Mpira wa miguu