Dkt.TUMAINI GURUMO AFURAHISHWA NA SERIKALI YA CHUO DAMISO KWENYE UUNDAJI WA TIMU YA CHUO

02 Feb, 2023
Dkt.TUMAINI GURUMO AFURAHISHWA NA SERIKALI YA CHUO DAMISO KWENYE UUNDAJI WA TIMU YA CHUO

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar Es Salaam (DMI) Dkt. Tumaini Gurumo ameipongeza Serikali ya wanafunzi wa chuo  (DAMISO) kwa kuandaa michezo ya mpira wa miguu kuanzia ngazi ya awali hadi kufikia fainali.

Dkt.Tumaini ametoa pongezi hizo leo kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Faundation vilivyopo Mnazi mmoja wakati alipokuwa akitoa zawadi kwa washindi mbalimbali baada ya kumaliza mashindano ya fainali yaliyohusisha wanafunzi kutoka ngazi ya cheti hadi Shahada ya Uzamili.

Dkt.Tumaini amesema kuwa Michezo mbali ya kuwa inaimarisha afya ya mwili na akili lakini pia ni sehemu pekee inaunganisha watu kwa pamoja na kujenga mahusiano ambayo wakati mwingine darasani si rahisi kuyajenga.

“Mimi ni mwanamichezo, napenda michezo, mwaliko huu nimeufurahia na nimefurahishwa zaidi kusikia Serikali ya wanafunzi imeaandaa mashindano haya, hii inaleta ari ya kutoa sapoti pale inapohitajika sababu mwanzo unakua mzuri”Alisema Dkt. Tumaini.

Mshauri wa wanafunzi Injia Regina Mbilinyi amemshukuru Mkuu wa chuo kukubali wito wa kuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo mbali na majukumu mengi aliyonayo  na kusema kuwa wanafunzi wamefurahishwa pia na uwepo wake kwenye mashindano hayo ya fainali.

Mratibu wa Michezo wa Chuo cha Bahari Mwl.Mansour Likamba amesema kuwa mchezo wa mpira ulianza kuchezwa kwa mwezi mmoja na nusu  hadi kufikia  leo fainali, Mashindano yalikua kwa madarasa yakijumuisha ngazi zote kuanzia Cheti hadi Shahada ya Uzamili kwa lengo la kutafuta timu ya mpira itakayokuwa inawakilisha Chuo kwenye mashindano mbalimbali.

Fainali ya leo imehusisha timu ya mpira ya  miguu ya madarasa ya SHIPPING na OIL&GAS and Mechatronics ambapo timu zote zimeundwa na wanafunzi  kuanzia ngazi ya cheti hadi Shahada ya Uzamili. Timu ya madarasa ya SHIPPING imeibuka kidedea kwa kuitandika OIL&GAS and Mechatronics magoli 3 kwa 2. Mshindi amekabidhiwa Tsh.320,000. na kombe pamoja na medali, mshindi wa pilia amekabidhiwa Tsh.200,000.

Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt. Tumaini Gurumo akiipongeza Serikali ya wanafunzi kwa kuweza kuandaa mashindano hayo.

Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt.Tumaini Gurumo  akizungumzia faida za michezo.

Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt.Tumaini Gurumo akikabidhi kombe na bahasha ya fedha kwa mwakilishi wa mshindi wa kwanza kwenye fainali hiyo.

Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt.Tumaini Gurumo akikabidhi kombe na bahasha ya fedha kwa mwakilishi wa mshindi wa kwanza kwenye fainali hiyo.

 

Mshauri wa wanafunzi Injinia Regina Mbilinyi akismhukuru Mkuu wa Chuo kwa kukubali wito wa kuwa Mgeni rasmi.

Mratibu wa Michezo Mwl. Mansour Likamba akizungumzia lengo la mashindano hayo na namna walivyoshirikisha madarasa yote kuunda timu.

Kaimu Mkuu wa Chuo Dkt.Tumaini Gurumo na viongozi wengine kwenye Picha ya Pamoja na washindi wa fainali baada ya Mashindano na zoezi la ugawaji wa zawadi kuisha.

Wanamichezo wakiwa uwanjani kuwania zawadi.

Shangwe ya timu ya Shippingi na washangiliaji baada ya mpira kuisha na kuibuka washindi.