Mfuko wa Elimu na Mafunzo ya Bahari (Matime Education and Training Fund – METFUND) Unawatangazia wadau wake wote kuhudhuria mkutano utakaofanyika tarehe 18 Mei, 2021 kuanziasaa 3:00 asubuhi katika ukumbi wa Karimjee ulioko jijini Dar es Salaam. Mgeni Rasmi katika mkutano huo ni Mh. AbubakariKunenge, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mada kuu itakayozungumzwa ni uwepo wa sheria ya Mfuko wa Elimu na Mafunzo ya Bahari, manufaa ya Mfukona Wajibu wa Wadau kwa Mfuko.

Wadau wa Mfuko ni pamoja na Wakala wote wa Forodha Tanzania, Wakala wote wa Meli Tanzania, Wamiliki wa Meli Tanzania, Taasisi za Elimu zinazotoa Mafunzo ya Bahari Tanzania, Taasisi na Makampuni yanayotoa Huduma za Bandari Tanzania, Mamlakaya Usimamizi wa Shughuli za Bahari Tanzania na Wamiliki wa Vituo vya Utafiti na Uvunaji wa Nishati Baharini.

“Kwa mawasiliano zaidi piga simu Na. +255 735 885 071 / +255 713 815 504 au tuma baruapepe kwa anuani ifuatayo; metfund.applications@dmi.ac.tz

Wadau wote mfike bila kukosa. Atakayesikia tangazo hili amtaarifu na mwenzake.